Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:35

Tanzania yaweka huduma ya intanet katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro


Mlima Kilimanjaro ulioko nchini Tanzania, Wilaya ya Hie, Dec. 10, 2009.
Mlima Kilimanjaro ulioko nchini Tanzania, Wilaya ya Hie, Dec. 10, 2009.

Tanzania imeanzisha huduma ya intanet yenye kasi zaidi katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro, ikiruhusu mtu yeyote mwenye simu za kisasa kutuma ujumbe wa Twitter, Instagram au WhatsApp wakiwa wanapanda mlima mrefu zaidi barani Afrika.

Kampuni mawasiliano inayomilikiwa na serikali ya Tanzania, imeweka mtandao wa broadband Jumanne katika mnyanyuko wa mita 3,720, huku Waziri wa Habari Nape Nnauye akisema ni tukio la kihistoria.

“Kabla ya kuwepo huduma hii, ilikuwa ni hatari kidogo kwa wageni na wabeba mizigo ambao walikuwa wakipanda mlima huo bila ya huduma ya intanet,” Nnauye alisema katika uzinduzi wa huduma hiyo, akiwa na maafisa wa serikali na watalii.

“Wageni wote wataweza kujiunga… (hadi kufikia) sehemu hii ya m lima,” alisema akiwa katika kituo cha mapumziko cha Horombo, moja ya kambi ukiwa unaelekea kileleni.

Alisema kuwa kilele cha mlima huo kilichopo mita 5,895 kitakuwa kimeunganishwa na intanet ifikapo mwisho wa mwaka.

Mwaka jana, serikali ya Tanzania ilitangaza mpango wa kujenga usafiri wa gari linalovutwa na waya katika upande wa kusini wa Kilimanjaro, iliyopelekea manung’uniko miongoni mwa wapanda mlima, makampuni yanayoendesha safari za upandaji mlima na wana mazingira.

Mlima Kilimanjaro ni chanzo muhimu cha mapato ya utalii nchini Tanzania na nchi jirani ya Kenya huku kukiwa na takriban watu 35,000 wanaojaribu kupanda mlima huo kufika kileleni kila mwaka.

Ikiwa imepewa kumbukumbu ya kudumu na maandiko ya Ernest Hemingway “The Snows of Kilimanjaro”, mlima huo ni sehemu ya hifadhi ya taifa na pia ni eneo la turathi za dunia iliyoorodheshwa na UNESCO.

Teknolojia imepenya zaidi katika ulimwengu wa upandaji milima, huku wanaopanda milima huko Mlima Everest wakipata urahisi wa kutumia Wifi, umeme wa jenereta na simu za kisasa zinaowezesha kutuma picha kwa wengine na kupiga simu za dharura iwapo kunatokea ajali.

Ikilinganishwa na wakati Edmund Hillary na Tenzing Norgay walipofika katika kilele cha mlima mrefu kuliko yote duniani May 29, 1953, habari hizo hazikuweza kuwafika maeneo mengine ya dunia mpaka mwezi June 2, wakati wa kutawazwa kwa Malikia Elizabeth II.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG