Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:41

Ajali ya basi Tanzania yauwa 13


Ajali ya basi iliyotokea Tanzania.
Ajali ya basi iliyotokea Tanzania.

Idadi ya vifo katika ajali ya basi la shule ya msingi King David iliyopo mkoani Mtwara nchini Tanzania imefikia 13 baada ya basi hilo kupinduka Jumanne asubuhi likiwa linaelekea shuleni.

Idadi ya vifo katika ajali ya basi la shule ya msingi King David iliyopo mkoani Mtwara nchini Tanzania imefikia 13 baada ya basi hilo kupinduka Jumanne asubuhi likiwa linaelekea shuleni.

Akizungumzia ajali hiyo iliyotokea mtaa wa mji mwema katika manispaa ya Mtwara mikindani majira ya saa mbili asubuhi , Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema chanzo cha ajali hiyo ni tatizo katika mfumo wa breki za gari.

Dr. Ahmad nyembea ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amesema kwamba wamepokea majeruhi kadhaa katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara kwa ajili ya kupatiwa matibabu huku wengine wakiwa katika hali mbaya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara BRIG.Gen.Marco Gaguti ametaka madereva kuwa makini na vyombo vya moto huku akihimiza pia kufuatwa kwa sheria za usalama barabarani

Baadhi ya mashuhuda wakiwemo wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo ya msingi ya Kinga David mkoani Mtwara wamezungumzia juu ya ajali hiyo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti kufuatia vifo hivyo ambavyo awali vilikuwa 10 lakini majeruhi wengine watatu wamefariki baadaye wakipatiwa matibabu na kufikisha idadi ya vifo 13.

XS
SM
MD
LG