Makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa juu ya idadi ya watu ulimwenguni yanatabiri kutakuwa na watu bilioni nane kwenye sayari ifikapo Novemba na kwamba idadi ya watu itaongezeka polepole hadi bilioni 8.5 ifikapo mwaka 2050 na zaidi ya bilioni 10 ifikapo mwaka 2080. Ongezeko hilo litakuja na athari kubwa za kiuchumi na kimazingira.
Ukuaji unaotarajiwa haujasambaa kwa usawa kote duniani. Baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na mashariki na kusini-mashariki mwa Asia yanatarajiwa kupungua kwa idadi ya watu, huku Amerika kaskazini na ulaya zikitarajiwa kukua kwa viwango vya chini sana. Sehemu kubwa ya ongezeko la watu linatarajiwa kutoka Afrika, kusini mwa jangwa la sahara na Asia ya kati, na kusini mashariki.
Hatua ya kupita alama bilioni 8 inaficha ukweli kwamba ulimwenguni, idadi ya watu inakua kwa kasi ndogo zaidi tangu miaka ya 1950. Theluthi mbili ya watu wote kwa sasa wanaishi katika maeneo ambayo kiwango cha uzazi, uzazi kwa kila mwanamke kimeshuka chini ya kiwango mabadala cha 2.1. Katika kesi nyingi viwango hivyo vinavyopungua vinatokana kwa sehemu na sera za serikali.
Ukuaji utalenga zaidi kati ya nchi nane; Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Misri, Ethiopia, India, Nigeria, Pakistan, na Ufilipino.
Kati ya nchi hizo nane inaelezwa kwamba nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara zitachangia zaidi ya nusu ya ongezeko la idadi ya watu duniani katika kipindi cha miaka 30 ijayo na hivyo kuunda kile maafisa wa Umoja wa Mataifa walichokiita uwezekano wa mgao wa idadi ya watu pamoja na sehemu ya watu wazima wenye umri wa kufanya kazi ikielezewa kama wale wenye umri wa kati ya miaka 26 na 64 wakiongezaka kama sehemu ya idadi ya watu.