Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:24

Mawaziri wa Utalii kutoka mataifa 50 wakutana Arusha kujadili sekta hiyo


Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na baadhi ya wadau wa seka ya Utalii.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na baadhi ya wadau wa seka ya Utalii.

Mawaziri wa utalii kutoka zaidi ya nchi 50 wanachama wa shirika la utalii Duniani na maafisa wa Kamisheni  ya Afrika Jumatano walikutana jijini Arusha Tanzania kujadili hali ya utalii ilivyo baada ya athari ya Janga la Covid 19 na pia  kuweka  mikakati mipya ya  kuendeleza sekta  hiyo.

Mkutano huo unaoshirikisha pia wataalam na watafiti wa masuala ya utalii duniani unafanyika wakati ambapo nchi mbalimbali duniani ambazo uchumi wake unategemea utalii ikiwemo Tanzania bado zinafanya jitihada kubwa kuimarisha sekta za utalii baada ya kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na Covid- 19.

Akifungua mkutano huo, Waziri Mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa alisema serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana kuimarisha sekta hiyo.

"Mwaka 2019 kabla ya mlipuko wa janga la Uviko 19 mapato yatokanayo na sekta ya utalii nchini Tanzania yalifikia dola za kimarekani Bilioni 2.9 na kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja milioni 2.5," alisema.

"Na katika kipindi hicho sekta ya utalii ilichangia wastani wa asilimia 17.2 ya pato ghafi la taifa," aliongeza.

Aidha waziri huyo Mkuu aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inaendelea kuongeza nguvu katika kulinda na kuhifadhi utalii wa rasilimali za asili na kuhakikisha unaendelea kuwanufaisha wananchi wa nchi hiyo na taifa kwa ujumla

"Hatua hii ni kielelezo tosha cha matokeo ya ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Jumuiya za kimataifa ikiwemo shirika la utali duniania hasa katika kuendelea sekta muhimu ya Utalii pamoja na masuala ya uhifadhi," alisema.

Kwa upande wake katibu wa shirika la utalii Duniani kamisheni ya Afrika Bw Zurab Pololikashvili alisema pamoja na changamoto zilizopo bado kuna umuhimu wa kuendelea na utalii na akaipongeza Tanzania kwa kuendelea kuimarisha misingi ya uhifadhi na utalii.

"Nafurahi na kufarijika kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, nchi ambayo inasifika kwa kitovu cha utali duniania ,baada ya janga la kovidi wakati sasa umefika wa kuinu sekta hii na kuhakikisha inasaidia masuala ya kiuchumi na kijamii," alisema.

Shirika la utalii duniani ambalo kwa sasa makao yake makuu yako Uhispania Lilianzishwa mwaka 1946 mjini London, nchini Uingereza na Tanzania ilijiunga na shirika hilo mwaka 1975.

-Ripoti imetayarishwa na Asraji Mvungi, VOA, Arusha, Tanzania

XS
SM
MD
LG