Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 12:32

Rais Samia Suluhu ni miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa sana duniani


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. PICHA: Ikulu ya Tanzania
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. PICHA: Ikulu ya Tanzania

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametajwa na jarida la Time 100, miongoni mwa viongozi 100 wenye ushawishi mkubwa duniani.

Rais Samia ameingia kwenye orodha hii kutokana na uongozi wake wa kipekee ambao ameonyesha tangu alipoingia madarakani mapema mwaka 2021 baada ya kifo cha John Pombe Magufuli.

Ameleta mabadiliko nchini Tanzania ikiwemo kuanzisha mazungumzo na wapinzani wake wa kisiasa. Amekutana na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema, Freeman Mbowe mara tatu. Mojawapo ya mambo ambayo wamezungumzia ni kuhusu maridhiano ya nchi na kufanya siasa kwa njia ya ustaarabu.

Wanaharakati Tanzania vile vile wamesema wkamba kuna juhudi za kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari chini ya utawala wa rais Samia ikilinganishwa na utawala wa Magufuli.

“Uongozi wake umekuwa kuvutia sana na wa kuigwa,” limesema jarida la Times.

Wengine walitajwa na jarida hilo ni rais wa Ukraine Volodymir Zelenskyy, Xi Jinping wa China, Vladimir Putini wa Russia, Xi Jinping wa China, Joe Biden wa Marekani, waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook.

Rais Samia amewateua wanawake katika wizara muhimu za nchi hiyo kama wizara ya afya, utalii na ulinzi.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG