Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:01

Tanzania : Polisi watofautiana juu ya kukamatwa kwa afisa wa LHRC


Tito Magoti afisa elimu wa kwa umma wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Tito Magoti afisa elimu wa kwa umma wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

Kamanda wa Polisi Kinondoni (RPC), Dar es Salaam, Tanzania, Musa Taibu ameeleza hana taarifa ya kukamatwa kwa afisa elimu wa kwa umma wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti.

Pia amefafanua kuwa katika eneo lake la utawala hakuna afisa mwenye taarifa za kukamatwa kwa ofisa huyo.

Hata hivyo vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Magoti anashikiliwa na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tangu Ijumaa iliyopita ya Desemba 20, 2019, baada ya kumkamata akiwa Mwenge Kinondoni jijini Dar es Salaam

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amekaririwa mara kadhaa na gazeti la Mwananchi akisema inamshikilia Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai.

Leo Jumatatu Desemba 23, 2019, Kamanda Taibu akizungumza na waandishi wa habari alizungumzia suala la Magoti baada ya kuulizwa na waandishi hao wakitaka kujua endapo anafahamu ofisa huyo wa LHRC amewekwa kituo gani.

Kamanda alijibu : "Kwa bahati mbaya sina taarifa hizi, nimeuliza wenzangu hakuna mwenye taarifa za kukamatwa kwa Tito kwenye himaya yangu."

XS
SM
MD
LG