Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:02

Kesi ya Kabendera mwandishi wa habari wa Tanzania imeahirishwa


Mwandishi wa habari Erick Kabendera akiwa ndani ya mahakama ya Kisutu huko Dar es Salaam, Tanzania, Aug. 5, 2019.
Mwandishi wa habari Erick Kabendera akiwa ndani ya mahakama ya Kisutu huko Dar es Salaam, Tanzania, Aug. 5, 2019.

Kabendera mwenye miaka 39 alikamatwa mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu akiwa nyumbani kwake kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu uraia wake. Baadae mashtaka yalibadilika na alishutumiwa kwa uasi, kutakasa fedha haramu na kupanga uhalifu

Kesi ya mwandishi wa habari wa Tanzania, Eric Kabendera aliyekamatwa mwezi Julai baada ya kumkosoa rais kwenye magazeti imeahirishwa tena mahakamani siku ya alhamis baada ya waendesha mashtaka kusema uchunguzi ungali unaendelea dhidi yake kwa mashtaka kadhaa ikiwemo uasi. Hivyo matumaini ya Kabendera kuachiwa kwa dhamana yalitoweka.

Kabendera alipowasili mahakamani alionekana mdhaifu na alitembea akiwa anachechemea. Mwanasheria wake, Jebra Kambole alisema mpango kuhusu matibabu ya afya yake bado haujafahamika.

“Ajenda kuhusu matibabu ya Kabendera imekuwa ni changamoto kuu kwa mahakama ambayo imearifiwa kwamba hali ya afya ya Kabendera sio nzuri. Mwanasheria huyo alisema hakimu alitoa maelezo ikiwemo kukutana na daktari ambaye anatoa huduma za matibabu gerezani ili Kabendera afanyiwe uchunguzi zaidi wa afya”.

Kambole alisema kikao kingine cha kesi yake itakayosikilizwa tena Septemba 18 mwaka huu italenga juu ya hali ya afya yake na mahakama huwenda ikatoa maelekezo zaidi wakati huo.

Erick Kabendera akiwasili mahakama ya Kisutu, Tanzania, Aug. 19, 2019.
Erick Kabendera akiwasili mahakama ya Kisutu, Tanzania, Aug. 19, 2019.

Kazi za Kabendera zimekuwa zikichapishwa na magazeti ya ndani na kimataifa. Mara nyingi anaandika kuhusu masuala ya siasa, biashara na viwanda barani Afrika kupitia magazeti ya The Guardian na The Times yote yana makao makuu yake Uingereza.

Baada ya kabendera kukamatwa, Kambole alisema mteja wake alikabiliwa na mashtaka ya uasi yakihusiana na makala aliyoandika kwenye jarida la The Economist ambapo alisema Rais John Magufuli wa Tanzania, anaharibu uhuru wa Tanzania.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu kamati ya kutetea waandishi wa habari-CPJ ilimjumuisha Kabendera katika kesi zake 10 za dharura ambazo zinahitaji mtazamo wa Dunia.

XS
SM
MD
LG