Ilukamba anachukuwa nafasi ya Bruno Tshibala aliyetumikia nafasi ya waziri mkuu tangu April 7 mwaka 2007, chini ya utawala wa rais mstaafu Joseph Kabila.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters Ilukamba kabla ya uteuzi huu alikuwa Mkuu wa Kampuni ya Reli ya Taifa nchini Congo inayojulikana kama SNCC. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko.
Wakati huo huo, maelfu ya watu Jumatatu wamemlaki kwa shangwe na vigelegele Moise Katumbi, mpinzani mkuu wa Rais mstaafu Joseph Kabila, alipowasili leo kwenye uwanja wa ndege mjini Lubumbabshi, akirejea nyumbani kutoka uhamishoni.
Katumbi mwenye umri wa miaka 54, mwanasiasa pia mfanyabiashara alikuwa gavana wa jimbo la Katanga kwa muda mrefu. Katumbi alikataliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa Disemba mwaka 2018, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 3 jela akiwa nje ya nchi.
Alikuwa anatuhumiwa kumiliki aridhi kinyume cha sheria, shutma ambazo alizikana. Lakini hukumu hiyo ilifutiliwa mbali na vyombo vya sheria vya DRC.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.