Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:50

DRC yarikodi kupungua kwa ukandamizaji kwa waandishi, wachapishaji wa habari


Rais Félix Tshisekedi
Rais Félix Tshisekedi

Matukio ya ukiukaji wa haki za waandishi na wachapishaji habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), vimepungua kwa asilimia 30 ukilinganisha na kipindi hiki mwaka 2018, linaelezea shirika la kutetea haki za waandishi wa habari (JED) nchini humo.

Pamoja na kuwepo mabadiliko hayo, bado shirika la JED linaelezea bado vyombo vya dola vinaendelea kuwatishia waandishi.

Ripoti ya shirika la kutetea haki za wandishi habari nchini Kongo, Journaliste En Danger, JED linaelezea kwamba toka mwanzoni mwa mwaka huu kuna visa 36 vya ukeukaji wa haki za upashaji habari nchini.

Kati ya matukio hayo ni kuakamtwa kwa waandishi habari na kufungwa kwa vyombo vya habari.

Toka kuapishwa kwa Rais Felix Tshisekedi kumeripotiwa visa 15. Tshivis Tshivuadi Katibu Mkuu wa shirika la JED amesema kwamba matukio hayo yamepungua kwa asilimia 30 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka 2018.

Kisa cha hivi karibuni ni kuhukumiwa kwa kifungo cha miezi 12 jela kwa mwandishi habari Steeve Mwanyo Iwewe, mjini Mbandaka, katika jimbo la Equateur katika kile jaji alichosema kuwa ni matamko ya matusi kwa gavana wa jimbo hilo.

Baada ya mwandishi huyo kukataa kutii amri ya Gavana ya kutompiga picha alipokuwa akijadiliana na waandamaji mjini huko.

Shirika la JED lilielezea kwamba vitisho zaidi dhidi ya waandishi wa habari viliripotiwa wakati wa kampeni ya uchaguzi amesema Claude Nyembwe.

Ripoti ya shirika la JED inaelezea kwamba kwa ujumla mwaka 2018, kuliripotiwa visa 121 vya ukeukaji wa haki za wandishi habari. JED imesema kwamba visa 54 vya wandishi habari walio kamatwa na kushikiliwa na polisi viliripotiwa kote nchini.

Wakati wa kuapishwa kwake kama Rais, Felix Tshisekedi aliahidi kuwakinga wandishi habari iliupashaji habari uchangie katika ujenzi wa taifa la haki.

"Serikali ambayo tutaunda hivi karibuni, itanzingatia vipaumbele kadhaa ikiwemo kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari ili upashaji habari uchukuwe nafasi muhimu katika ujenzi wa taifa letu," alisema Rais.

Shirika la kutetea haki za waandishi wa habari, Journaliste en Danger, limesikitika kuona kwamba baadhi ya wahusika na via vya ukeukaji wa haki za upashaji habari hawapewe adhabu yeyote.

JED ilielezea kwamba wandishi habari 30 walivamiwa ao kujeruhiwa na polisi mnamo mwaka 2018. Matukio mengi yalitokea hasa wakati wa manadamano ya upinzani ama mashirika ya kiraia.

Ikiwa kwa upande mmoja uhuru wa upashaji habari umeahakikishwa nchini lakini bado badhi ya waandishi pia wametuhumiwa kutoheshimu utovu wa nidhamu. Delion Kimbulungu ni mtaalamu wa maswala ya upashaji habari nchini.

Shirika la kimataifa la waandishi wasiokuwa na mipaka, Reporter Sans Frontieres, kwenye ripoti yake ya mwaka uliopita iliiweka Congo kwenye nafasi ya 154 miongoni mwa nchi 180 katika jadwali la uhuru wa upashaji habari. Miaka 11 iliyopita waandishi habari zaidi ya 10 waliuawa nchini hapa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Saleh Mwanamilongo, DRC

XS
SM
MD
LG