Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:24

SADC inaitaka DRC kurudia kuhesabu kura za urais


Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa-SADC
Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa-SADC

Wakati huo huo kanisa Katoliki Congo linasema kura zilizokusanywa na timu yake yenye waangalizi 40,000 inaonesha mshindi tofauti kutoka yule aliyetangazwa na tume ya uchaguzi bila ya kusema ni nani

Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika-SADC ilisema Jumapili kwamba Jamhuri ya kidemocrasi ya Congo-DRC inatakiwa kurudia kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais ambapo mgombea mmoja anasema aliibiwa kura.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters uchaguzi wa Disemba 30 mwaka jana ungeleta makabidhiano ya kwanza ya madaraka nchini Congo kwa njia ya kidemokrasia tangu nchi hiyo ipate uhuru miaka 59 na mwanzo wa enzi mpya kufuatia miaka 18 ya utawala wa Rais Joseph Kabila. Lakini mgombea Martin Fayulu anadai kwamba alipata ushindi mkubwa na kwamba mshindi rasmi kiongozi wa upinzani Felix Tshisekedi alikula njama na Kabila ili Tshisekedi atangazwe mshindi. Madai ambayo Tshisekedi na Kabila wanakanusha.

Kanisa Katoliki Congo linasema kwamba kura zilizokusanywa na timu yake yenye waangalizi 40,000 inaonesha mshindi tofauti kutoka yule aliyetangazwa na tume ya uchaguzi bila ya kusema ni nani. Mabishano ya baada ya uchaguzi kwenye nchi hiyo kubwa yenye utajiri wa madini na watu milioni 80 yamewafanya wengi kukhofia kurudi kwa ghasia za vita vya wenyewe kwa wenyewe ambazo zimeuwa mamilioni ya watu tangu miaka ya 1990.

XS
SM
MD
LG