Kauli hiyo imeongeza shinikizo kwa sauti nyingine zinazoitaka Kinshasa kurekebisha mzozo huo wa matokeo ya uchaguzi ambao unaweza kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.
Hata hivyo upigaji kura wa December 30, 2018, ulisifiwa kuwa ni hatua ya kwanza ya kidemorkasia ya makabidhiano ya madaraka kwa njia ya uchaguzi katika kipindi cha miongo kadhaa tangu nchi hiyo ijipatie uhuru kutoka Ubelgiji.
Uchaguzi huu pia ni mwanzo wa enzi mpya baada ya nchi hiyo kuwa chini ya utawala uliogubikwa na vurugu kwa miaka 18 ya utawala wa Rais Joseph Kabila.
Lakini makundi yanayofuatilia uchaguzi yalizungumzia mapungufu mbalimbali ya uchaguzi ikiwemo mashine za kupigia kura ambazo zilikuwa na matatizo.
Pia kumekuwa na malalamiko mbalimbali kuhusu utendaji wa viwango vya chini kwenye vituo vya kupigia kura, na kugubikwa na mazungumzo ya masuala ya kidemokrasia katika nchi hiyo yenye watu takriban milioni 80. Shirika hilo lina nchi wanachama 12 ikiwemo DRC.