Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:04

Mkuu wa tume ya uchaguzi DRC aishauri UN


Corneille Nangaa
Corneille Nangaa

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Corneille Nangaa, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia mawasiliano ya Satellite kuwa Congo ina njia mbili : kukubali matokeo hayo au kuyafuta.

Amesema iwapo matokeo yatafutwa, nchi haitakuwa na rais mpya mpaka uchaguzi mwengine utakapo anadaliwa.

Mwandishi wa Sauti ya America ( VOA ) Umoja wa Mataifa anaripoti kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana New York Ijumaa kuzungumzia uchaguzi wa Congo.

Rais aliyeko madarakani Joseph Kabila tayari ameendelea kutawala kwa zaidi ya miaka miwili baada ya muhula wake kumalizika. Alikuwa tayari amejitayarisha kuachia madaraka mwezi huu baada ya miezi 18 madarakani, mara tu rais mpya atakapo chaguliwa.

Katika uchaguzi huo, Kabila alimuunga mkono waziri wake wa mambo ya ndani wa zamani, Emmanuel Shadary, ambaye alichukuwa nafasi ya tatu. Wafuasi wa Fayulu wamemtuhumu Kabila kwa kufanya makubaliano na tume ya uchaguzi kumnyima mgombea wao ushindi wa urais.

DRC haijawahi kuwa na kubadilishana kwa madaraka kwa njia ya amani tangu ilipopata uhuru kutoka Ubelgiji 1960.

Fayulu apinga matokeo

Mgombea urais DRC Martin Fayulu amesema atafungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mmoja wa wapinzani wake katika kinyang’anyiro hicho.

Akizungumza na VOA, Fayulu amesema atakwenda Mahakama ya Katiba Kinshasa Jumamosi kushinikiza kura zihisabiwe upya.

Lakini, Fayulu alisema anashaka iwapo mahakama hiyo itabadilisha matokeo yaliyo tangazwa na tume ya uchaguzi ya Congo.

Tume hiyo imemtangaza Felix Tshisekedi, mtoto wa kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Disemba 30. Imesema Fayulu, mfanyabiashara ambaye anaungwa mkono na muungano wa vyama vya upinzani alikuwa namba mbili.

Hata hivyo, timu ya Kampeni ya Fayulu imesema ina majumuisho ya kura yanayo onyesha kuwa mgombea wao alishinda kwa kura asilimia 61.

Kanisa Katoliki na wanadiplomasia wa nchi za nje pia wamehoji matokeo ya uchaguzi huo. Kanisa limesema Alhamisi kuwa hisabu rasmi iliyotolewa hailingani na majumuisho ya kura zilizo kusanywa na waangalizi wake 40,000 waliosambazwa nchini kote.

XS
SM
MD
LG