Matokeo ya awali yameonyesha kuwa yeye anaongoza katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya mgombea wa muungano wa upinzani Martin Fayulu na yule wa muungano wa chama tawala Emmanuel Shadary.
Mapema majira ya alfajiri Alhamisi mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi DRC-CENI, Corneille Nangaa ametangaza Tshisekedi “alipata kura asilimia 38.57”.
Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo akiwa katika makao makuu ya tume ya uchaguzi mjini Kinshasa na kwanza anaelezea kile alichosema mwenyekiti wa CENI.
Atakapo thibitishwa Tshisekedi atakuwa mshindani mpinzani wa kwanza kushinda tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.
Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya miaka 18 ya uongozi wake.
Alikuwa ameahidi kuwepo ili kubadilishana madaraka kwa njia ya utulivu huko DRC tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Ubelgiji mwaka 1960.