Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:08

Serikali ya Biden kuendeleza demokrasia kwa njia ya amani


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Antony Blinken anasema utawala wa Biden unataka kuendeleza demokrasia katika nchi za nje na wala sio utumiaji nguvu za kijeshi inayogharimu maisha na fedha nyingi.

Akizungumza juu ya malengo ya sera za kigeni za utawala mpya hapo jana katika wizara ya mambo ya nje Blinken amesema utumaij nguvu imeshindwa kuleta mafanikio mnamo miaka ya nyuma.

Jeshi la Marekani likiwa limeshakamilisha karibu miaka 30 ya kuzuia mapigano nchini Irak na miaka 20 nchini Afghanistan, wakosowaji wa uingiliaji kati kijeshi wanatoa tena wito kwa serikali ya Washington kuwarudisha nyumbani wanajeshi wake na kuachana na juhudi za mabadiliko ya utawala mnamo sku za mbele.

Majeshi ya Marekani nchini Iraq
Majeshi ya Marekani nchini Iraq

Akifafanua sera za kigeni za utawala mpya, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Blinken amesema utawala wa Biden utabuni njia yake, katika kujaribu kuendeleza demokrasia kwa mifano na wala sio kwa utumiaji nguvu.

Blinken anaeleza : "Tutahamasisha tabia za kidemokrasia, lakini hatutaendeleza deokrasia kupitia uingiliaji kati wa kijeshi wenye kugharimu fedha nyingi au kwa kujaribu kupindua serikali za kimabavu kwa nguvu. Tumeshajaribu mbinu hizi mnamo miaka ya nyuma. Lakini hata tukiwa na nia njema gani hazija weza kufanya kazi."

Blinken anasema uingiliaji kati kijeshi umeipatia demokrasia sifa mbaya na kutokua ten na imani ya Wamarekani. Alihaidi kwamba utawala wa Biden utafanya mambo kwa njia tofauti, ikiwa ni pamoja na kuimarisha wazo hapa nyumbani kwamba demokrasia ni jambo muhimu katika sera za kigeni.

Mwanadiplomasa huyo mkuu amesema China ndio tishio kubwa kwa sababu ndio nchi pekee yenye nguvu kuleta changamoto na kuvuruga mfumo wa uwazi wa kimataifa. Amesema ni lazima kwa Washington kuikabili Bejing ikiwa na msimamo wenye nguvu.

Rais Xi Jinping
Rais Xi Jinping

"Hiyo itahitaji kufanya kazi na washirika wetu na wala sio kuwatenganisha, kwa sababu nguvu zetu kwa pamoja zitasababisha hali kua ngumu kwa China kudharau. Ina hitaji kujishughulisha kwa njia ya kidiplomasia na kuimarisha uhusiano na mashirika ya kimataifa, kwa sababu pale ambapo tumejiondoa China imejiingiza," amesema Waziri Blinken.

US General Lloyd Austin
US General Lloyd Austin

Akikiri kwamba yeye pamoja na maafisa wengine wa utawala mpya pamoja na Joe Biden walifanya kazi chini ya Rais Barak Obama, hata hivyo Blinken alikataa wazo kwamba timu ya sasa ni kurudishwa upya utawala wa Obama. Amesema dunia imebadlika tangu enzi ya Obama, muda umepita na Biden atachukulia masuala ya dunia kwa mtizamo mpya.

XS
SM
MD
LG