Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:15

Iraki : Shambulizi la roketi 10 zalenga kambi ya jeshi ya Al-Asad


KIkosi cha anga cha Al-Asad, Iraki.
KIkosi cha anga cha Al-Asad, Iraki.

Muungano unaoongozwa na Marekani nchini Iraq umeeleza Jumatano kumefanyika shambulizi la roketi lililolenga kambi ya jeshi ambayo inatumiwa na vikosi vya muungano.

Msemaji wa muungano huo Kanali Wayne Marotto amesema kulikuwa na roketi 10 zilizo fyatuliwa katika kambi ya jeshi la anga la Al-Asad.

Hakuna taarifa zozote za vifo mpaka hivi sasa. Shambulizi hilo limefanyika baada ya kupita wiki mbili toka kutokea tukio lingine la roketi kurushwa katika kambi ya jeshi iliyopo kaskazini mwa Ifaq na kumuua mkandarasi ambaye ni raia ina kujeruhi wanajeshi wa Marekani.

Athari ya roketi iliyotua katika kambi ya kikosi cha anga cha Al Asaad cha majeshi ya ushirika yanayo ongozwa na Marekani, Iraq
Athari ya roketi iliyotua katika kambi ya kikosi cha anga cha Al Asaad cha majeshi ya ushirika yanayo ongozwa na Marekani, Iraq

Mashambulizi ya Febuari 16 yalichochea Marekani kufanya mashambulizi ya anga yakilienga Syria ambapo Pentagon ilieleza kuwa ndiko kuliko pangwa mashambulizi mfululizo katika kambi za jeshi nchini Iraq.

XS
SM
MD
LG