Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:59

Wabunge Marekani wamesitisha kikao cha bunge kutokana na onyo la usalama


Muonekana wa sasa wa jengo la bunge la Marekani
Muonekana wa sasa wa jengo la bunge la Marekani

Bunge lilikua limepanga kujadili na kupiga kura Alhamis ili kupasisha mswada wa sheria kuhusu mageuzi kwenye idara ya  polisi Marekani

Baraza la wawakilishi la Marekani limesitisha kikao kilichopangwa kufanyika Alhamisi baada ya polisi wa kulinda usalama wa bunge kuonya Jumatano kuhusu uwezekano wa njama iliopangwa na kundi la wanamgambo kuvamia jengo la bunge, tishio ambalo linakumbusha shambulizi baya lililotokea Januari 6 mwaka huu.

Bunge lilikua limepanga kujadili na kupiga kura Alhamis ili kupasisha mswada wa sheria kuhusu mageuzi kwenye idara ya polisi. Lakini mshauri wa mbunge mmoja wa Democrat amesema, onyo la polisi kufuatia taarifa za idara ya ujasusi kwamba kundi la wanamgambo ambalo halijatambulika linaweza kutishia usalama, limechangia kubadili ratiba ya baraza la wawakilishi.

Wafuasi wa Donald Trump walishambulia jengo la bunge, Jan. 6, 2021.
Wafuasi wa Donald Trump walishambulia jengo la bunge, Jan. 6, 2021.

Viongozi walisema makundi yenye itikadi kali ya mrengo wa kulia ni miongoni mwa wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump, waliovamia jengo la bunge mwezi Januari wakitaka kukwamisha zoezi la wabunge kurasimisha ushindi wa Rais Joe Biden kufuatia uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka jana.

March 4 ni tarehe ambapo wapanga njama wa mrengo wa kulia waliotoa madai yasiyokua na msingi kwamba Donald Trump alishinda uchaguzi wa Novemba 3, wanaamini kuwa ndio siku ambapo Trump ataapishwa kuongoza kwa muhula wa pili.

Ofisi ya mwanasheria mkuu imekwisha washtaki zaidi ya watu 300 walioshiriki kwenye uvamizi wa jengo la bunge, ambapo watu watano akiwemo afisa wa polisi waliuwawa katika uvamizi huo.

XS
SM
MD
LG