Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:12

Trump: Sina mpango wa kujaribu kuanzisha chama kipya


Rais wa zamani Marekani Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa kihafidhina CPAC huko Orlando, Feb 28, 2021
Rais wa zamani Marekani Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa kihafidhina CPAC huko Orlando, Feb 28, 2021

Trump alisema katika hotuba yake kwenye kongamano la wanasiasa wenye msimamo wa kihafidhina katika jimbo la Florida "harakati zetu za wamarekani wazalendo na wachapa kazi kwa bidii, zinaanza hivi sasa, na mwishowe tutashinda"

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alidokeza Jumapili uwezekano wa kugombea tena urais mwaka wa 2024 na kumshambulia Rais Joe Biden na kurejelea madai yake ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa 2020 na kudai kwamba alishinda uchaguzi huo. Trump alijitokeza na kuzungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu aondoke White House wiki sita zilizopita.

“Harakati zetu za wamarekani wazalendo na wachapa kazi kwa bidii, zinaanza hivi sasa, na mwishowe tutashinda. Tutashinda”, Trump alisema katika hotuba yake kwenye kongamano la wanasiasa wenye msimamo wa kihafidhina mjini Orlando, katika jimbo la Florida.

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa CPAC
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa CPAC

Akipinga kukubali kwamba alishindwa kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 3 Novemba mwaka jana, Trump alikosoa vikali uongozi wa wiki za mwanzo za mrithi wake mDemocrat Joe Biden na kupendekeza kuwa anaweza kugombea tena.

Katika wiki za mwisho za uongozi wa Trump wafuasi wake walishambulia jengo la bunge la Marekani tarehe 6 Januari katika jaribio la kulizuia bunge kurasimisha ushindi wa Joe Biden, ushindi ambao Trump anaendelea kusema bila ushahidi wowote kwamba uligubikwa na wizi mkubwa wa kura.

Trump alitangaza kwamba chama cha Republican kimeungana na hana mpango wa kujaribu kuanzisha chama kipya wazo ambalo aliwahi kujadili na washauri wake katika miezi iliyopita.

XS
SM
MD
LG