Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:02

Russia yaripotiwa kuwahamisha watoto zaidi 2,400 wa Ukraine kwenda Belarus


Eneo la maduka yaliyoharibiwa na mabomu ya Russia huko Odesa Mei 10, 2022. Picha na REUTERS/Igor Tkachenko
Eneo la maduka yaliyoharibiwa na mabomu ya Russia huko Odesa Mei 10, 2022. Picha na REUTERS/Igor Tkachenko

Zaidi ya watoto 2,400 wa Ukraine wamepelekwa Belarus tangu Russia ilipoivamia Ukraine mwaka 2022, kulingana na utafiti mpya uliochapishwa siku ya Alhamisi na Chuo Kikuu cha Yale.

Matokeo ya Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Shule ya Afya ya Umma ya chuo kikuu cha Yale ni ya kina zaidi kuhusiana na jukumu la Belarus kwa Russia kuwalazimisha kwa lazima wa watoto wa Ukraine.

Ripoti hiyo iligundua kwamba watoto wa Ukraine, wenye umri wa miaka 6 hadi 17, walikuwa wamesafirishwa kutoka miji isiyopungua 17 katika eneo la Ukraine linalokaliwa kimabavu na Russia.

Yale ilibaini zaidi ya watoto 2,000 waliokuwa wamesafirishwa kwenda kituo cha watoto cha Dubrava katika mkoa wa Minsk wa Belarusi kati ya mwezi Septemba 2022 na Mei 2023. Zaidi ya watoto 390 walipelekwa kwenye vituo vingine 12, ripoti hiyo ilisema.

Hiyo ni juu ya watoto takribani 20,000 wa Ukraine ambao walichukuliwa kwa nguvu kutoka Ukraine kwenda Russia tangu vita kuanza, kulingana na Kateryna Rashevska, mtaalam wa sheria katika Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Kikanda mjini Kyiv.

Waendesha mashitaka wa uhalifu wa kivita kwa Ukraine wanachunguza uhamisho wa lazima wa watoto wa Ukraine yakiwa kama mauaji ya halaiki.

Wakati huohuo, mashambulizi ya makombora ya Russia siku ya Alhamisi yaliwauwa watu wawili na kuwajeruhi takriban 12 katika eneo la Kherson kusini mwa Ukraine, maafisa wa eneo hilo walisema.

Forum

XS
SM
MD
LG