Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:49

Ukraine haiwezi kumudu kukwama katika vita na Russia- Zelenskyy


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Ukraine Septemba 20, 2023. Picha na ANGELA WEISS / AFP
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Ukraine Septemba 20, 2023. Picha na ANGELA WEISS / AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameonya kwamba kukwama kwa vita vya nchi yake dhidi ya Russia kutazua "volcano ambayo imelala lakini bila shaka italipuka."

"Hatuwezi kumudu kukwama kwa aina yoyote," Zelenskyy aliwaambia waandishi wa habari wa Afrika mjini Kyiv siku ya Jumatano. "Kama tunataka kumaliza vita, lazima tuvikomeshe. Tumalizie kwa heshima ili dunia nzima ijue kwamba yeyote aliyekuja, atakamatwa na kuuawa, ni kuwajibika."

Kulingana na rais wa Ukraine, iwapo vita hivyo vitakwama, vizazi vijavyo vya Waukraine vitalazimika kupigana, kwa sababu Russia "itakuja tena ikiwa haitawekwa mahali pake."

Maoni ya Zelenskyy yalikuja wiki mbili baada ya Jenerali Valery Zaluzhny, kamanda mkuu wa jeshi la Ukraine, kuliambia gazeti la The Economist kwamba vita "vimefikia kiwango cha teknolojia ambacho kinatukwamisha."

Zelenskyy alikiri kwamba hali katika uwanja wa vita bado ni ngumu sana lakini akasema haamini kwamba vita vimefikia kikomo. Alisisitiza kuwa Ukraine haitajadiliana na Russia hadi itakapojiondoa kabisa katika maeneo ya Ukraine.

Pia siku ya Jumatano, Zelenskyy alizungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Kulingana na idara ya habari ya rais wa Ukraine, viongozi hao wawili walizungumzia kuhusu hali ya uwanja wa vita, ushirikiano wa kiulinzi kwa kusisitiza kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine na "kuongeza uwezo wa vikundi vya vinavyozunguka kupambana na ndge zisizokuwa na rubani [drones]."

Forum

XS
SM
MD
LG