Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:29

Russia yaripoti shambulizi la ndege zisizo na rubani mjini Moscow


Jengo lililoharibiwa katika mji wa "Moscow City" wilaya ya kibiashara baada ya kuripotiwa shambulizi la droni Moscow, Russia, Aug. 1, 2023. Jengo hilo tayari lilikuwa limeshambuliwa kwa droni siku mbili zilizopita.
Jengo lililoharibiwa katika mji wa "Moscow City" wilaya ya kibiashara baada ya kuripotiwa shambulizi la droni Moscow, Russia, Aug. 1, 2023. Jengo hilo tayari lilikuwa limeshambuliwa kwa droni siku mbili zilizopita.

Maafisa wa Russia walisema Jumanne mifumo ya ulinzi wa anga ilitungua ndege kadhaa za Ukraine zisizo kuwa na rubani zilizokuwa zimelenga kuishambulia Moscow, huku mabaki ya moja ya droni hizo ikiangukia katika jengo refu la ghorofa katika mji mkuu wa Russia.

Meya wa Moscow Sergei Sobyanin alisema kupitia Telegram jengo hilo ni lile lile ambalo lilishambuliwa katika shambulizi jingine la droni Jumapili.

Hakuna ripoti za majeruhi kutokana na shambulizi hilo la Jumanne.

Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema Jumanne kuwa majeshi yake yalizima shambulizi la droni tatu za Ukraine zilizotokea upande wa baharini ambazo zililenga kushambulia meli mbili za doria za Russia katika bahari ya Black Sea.

Russia ilisema shambulizi hilo lilitokea kiasi cha kilomita 340 kusini magharibi mwa Sevastopol.

Mashambulizi yaliyofanywa na Russia

Maafisa katika mji wa Kherson ulioko kusini mwa Ukraine walisema shambulizi la Russia Jumanne lilipiga hospitali, na kumuua daktari na kumjeruhi muuguzi.

Wafanyakazi wa huduma za dharura wakiwa katika eneo la shambulizi la kombora lililopiga jengo la makazi ya watu huko Kryvyi Rih, Ukraine, Julai 31, 2023. (AP Photo/Libkos)
Wafanyakazi wa huduma za dharura wakiwa katika eneo la shambulizi la kombora lililopiga jengo la makazi ya watu huko Kryvyi Rih, Ukraine, Julai 31, 2023. (AP Photo/Libkos)

Katika mkoa wa Kharkiv, maafisa walisema Jumanne kuwa shambulizi la Russia likitumia droni zilizotengenezwa Iran zilipiga jengo katika taasisi ya elimu na jengo jingine kwenye kituo cha michezo.

Mashambulizi ya Russia dhidi ya miji ya Ukraine yamesababisha vifo na majeruhi, ikimchochea Rais Volodymyr Zelenskyy kusisitiza haja ya Ukraine kupatiwa silaha za masafa marefu.

Watu wasiopungua sita waliuawa na makombora mawili ya Russia ambayo yalipiga mji wa Kryvyi Rih kusini mwa Ukraine, mji alikozaliwa Zelenskyy, maafisa wa Ukraine walisema Jumatatu.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG