Mkutano huo wa siku mnbili huko Saint Petersburg alikozaliwa Putin unachunguzwa kama kipimo cha uungwaji mkono wake barani Afrika ambapo anaendelea kuungwa mkono licha ya kutengwa kimataifa kulikosababishwa na uvamizi wake wa kijeshi nchini Ukraine mwaka jana.
Wiki iliyopita, Russia ilikataa kuongeza mkataba ambao ulihusika na mauzo ya nafaka ya Ukraine kupitia Black Sea kufika masoko ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Afrika na kupunguza shinikizo la bei ya vyakula.
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo Putin alisema Russia inaweza kutafuta mbadala wa nafaka ya Ukraine na kuahidi kupeleka nafaka katika nchi sita za Afrika.
Forum