Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:08

Ulaya haitavumilia uchokozi nchini Ukraine au Indo-Pacific; anasema Von der Leyen


Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen. Manila, July 31, 2023.
Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen. Manila, July 31, 2023.

Von der Leyen alizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. baada ya kufanya mazungumzo mjini Manila ambayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na usalama

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen alionya Jumatatu kwamba Ulaya haitavumilia uchokozi nchini Ukraine au katika eneo la Indo-Pacific wakati akithibitisha tena EU kutambua uamuzi wa usuluhishi wa 2016 ambao ulibatilisha madai ya China ya upanuzi wake katika South China Sea.

Von der Leyen alizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. baada ya kufanya mazungumzo mjini Manila ambayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kiuchumi na usalama.

Viongozi hao wametangaza kuwa jumuiya hiyo yenye mataifa 27 itaanza tena mazungumzo na Ufilipino kwa makubaliano ya biashara huru yaliyokwama mwaka 2017 chini ya mtangulizi wa Marcos, Rodrigo Duterte.

Ursula alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa usalama akitaja uvamizi wa Russia nchini Ukraine, ambao alisema unaonyesha jinsi viongozi wa kiimla wako tayari kuchukua hatua kwa vitisho vyao.

Forum

XS
SM
MD
LG