Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:31

'Ukraine bado inazo njia mbadala nyingi wanazoweza kuchagua kujibu mashambulizi ya Russia,' asema Lloyd


Takriban droni 1,700 zinatayarishwa kupelekwa katika mstari wa mbele vitani huko Ukraine kutumika kukabiliana na uchokozi wa majeshi ya Russia huko Kyiv, Ukraine, Julai 25, 2023.
Takriban droni 1,700 zinatayarishwa kupelekwa katika mstari wa mbele vitani huko Ukraine kutumika kukabiliana na uchokozi wa majeshi ya Russia huko Kyiv, Ukraine, Julai 25, 2023.

Maafisa wa wizara ya ulinzi ya Marekani wakiangalia Ukraine ikipiga hatua polepole katika kujibu mashambulizi dhidi ya Russia hawako tayari kuelezea wasiwasi wa aina yoyote, licha ya kutokuwepo mafanikio makubwa.

Kulikuwa na matumaini kuwa kuongezeka kwa vifaru vya kivita na magari yenye silaha, na pia silaha nyingine mpya, mifumo ya makombora na mizinga ingeweza kulifanya jeshi la Kyiv kuweza kupenya katika ngome za Russia.

Akizungumza wakati wa ziara yake huko Papua New Guinea Alhamisi, hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema Ukraine bado ina muda wa kutosha.

“Bado ziko njia mbadala nyingi wanazoweza kuchagua,” Austin aliuambia mkutano wa waandishi akiwa na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape.

“Wamekuwa na makusudio maalum. Wamekuwa wakiweka akiba ya wafanyakazi na vifaa,” alieleza. “Nafikiri unaweza kuwatarajia kuendelea kuweka shinikizo [dhidi ya Russia].”

Maafisa wa Ukraine wamelaumu aina ya kujihami kwa Russia, hasa mabomu yanayopandikizwa na majeshi ya Russia wakifanya hivi katika kipindi cha baridi, kwa ajili ya kuwazuia wasisonge mbele.

Maafisa waandamizi wa jeshi la Marekani wanakiri kuwa mabomu yaliyopandikizwa na Russia ni tatizo.

Hata hivyo, maafisa wa sasa na zamani, na pia baadhi ya wachambuzi, wanaeleza kero yao kuwa makamanda wa Ukraine wameegemea katika mbinu za kizamani za Soviet badala ya kufuata nadharia za Marekani ambazo zingeweza kuongeza kasi ya mashambulizi yanayofanywa na Kyiv.

Austin alitahadharisha, hata hivyo, kuwa baadhi ya matarajio kuhusu mashambulizi yanayofanywa na Ukraine inawezekana yaliwekewa matumaini makubwa.

“Tulisema wakati huu wote kuwa haya yatakuwa mapambano magumu na yatakuwa ni ya muda mrefu,” alisema. “Tumeona kwa kiasi kubwa namna ilivyotokea.”

Forum

XS
SM
MD
LG