Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:06

Uingereza yasema Russia inawezekana inajiandaa 'kutekeleza kizuizi kwa Ukraine'

FILE - Picha hii ilichapishwa na ofisi ya habari ya Wizara ya Ulinzi ya Russia Aprili 14, 2021 Inaonyesha meli ya jeshi la majini la Russia ikifanya mazoezi ya kijeshi katika bahari ya Black Sea.
FILE - Picha hii ilichapishwa na ofisi ya habari ya Wizara ya Ulinzi ya Russia Aprili 14, 2021 Inaonyesha meli ya jeshi la majini la Russia ikifanya mazoezi ya kijeshi katika bahari ya Black Sea.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumatano kuwa Russia imebadilisha harakati zake za jeshi la majini katika bahari ya Black Sea, ikiongeza kuwa kuna uwezekano majeshi ya Russia yanajiandaa “kutekeleza kizuizi kwa Ukraine.”

Wiki iliyopita, Russia ilijitoa katika mkataba wa karibu mwaka mmoja uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki ulioruhusu usafirishaji salama kwa njia ya meli nafaka kutoka bandari za Ukraine zilizoko bahari ya Black Sea.

Kabla ya makubaliano hayo, uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulisimamisha usafirishaji wa nafaka nje ya nchi, na kufanya mgogoro wa hali ya chakula ulimwenguni kuwa mbaya zaidi.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika taarifa yake mpya ya kila siku kuwa meli ya kivita ya Russia Sergey Kotov ilipelekwa katika bahari ya Black Sea kufanya doria katika njia ya meli kati ya Bosporus Strait na bandari ya kusini mwa Ukraine ya Odesa.

“Kuna uwezekano wa kweli kuwa itafanya sehemu ya kikosi kazi kitakacho zizuia meli za biashara ambazo Russia inaamini zinaelekea Ukraine,” wizara ya Uingereza ilisema.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na ripoti ya mashirika ya habari ya AP, AFP, na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG