Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:46

Rais Putin kujadili masuala ya Ukraine na viongozi wa Afrika


FILE PHOTO: Mkutano wa Russia-Afrika huko Sochi
FILE PHOTO: Mkutano wa Russia-Afrika huko Sochi

Rais wa Russia Vladimir Putin ataijadili Ukraine na viongozi wa mataifa ya Afrika, ambao watakusanyika kwa ajili ya mkutano wa Russia na Afrika ambao utafanyika Saint Petersburg kesho.

Julai 29, Vladimir Putin anatarajiwa kuwa na chakula cha mchana huku akifanya mkutano na kundi la viongozi wa nchi za Afrika kuhusu masuala ya Ukraine, Kremlin imesema katika taarifa yake.

Viongozi kadhaa wa Kiafrika akiwemo Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa wanatarajiwa katika mkutano huo ambao utafanyika Alhamisi na Ijumaa katika mji wa Saint Petersburg anakotokea Putin.

FILE PHOTO: Rais Vladimir Putin akiwa na Rais Cyril Ramaphosa
FILE PHOTO: Rais Vladimir Putin akiwa na Rais Cyril Ramaphosa

Mwishoni mwa mkutano huo azimio litapitishwa kuelezea “mwelekeo wa pamoja kwa maendeleo ya ushirikiano wa Russia na Afrika,” Kremlin iliongezea.


Mwisho wa makubaliano ambayo yaliruhusu mauzo ya nje ya nafaka za Ukraine kupitia bahari ya Black Sea kwenye masoko ya dunia, ikiwemo Afrika, ni suala ambalo linatarajiwa kutawala ajenda ya mkutano huo.

Katika siku chache za mwisho, Moscow ilitaka kuwahakikishia tena washirika wa kiafrika, ikisema inaelewa “wasiwasi” wao katika suala hili.

Mtalaamu wa chuo kikuu cha Russia cha HSE kwa masuala ya Afrika ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mkutano huo wa viongozi ni “hatua muhimu sana” kuelekea “kuunganishwa upya kwa mahusiano” kati ya Russia na nchi za Afrika.

Ramani ya Afrika
Ramani ya Afrika

Vsevolod Sviridov, Mtaalamu, Kituo cha Masuala ya Afrika, Chuo Kikuu cha HSE anasema, “lengo kuu la mkutano wa pili ni kuona kitu gani kimefanyika katika miaka ya karibuni baada ya mkutano wa kwanza.

Uchumi wa dunia na siasa zimebadilika. Kwanza, kulikuwa na janga la Covid 19, halafu operesheni maalum ya kijeshi uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulianza. Muundo wa kazi ambao Russia na Afrika wataingiliana nao umebadilika sana. Kwahiyo, ni dhahiri, kuna haja ya kuunganishwa upya uhusiano kati ya Russia na nchi za kiafrika. Ni muhimu kutafuta njia muafaka, kueleza kwa kila mmoja mwelekeo kuhusu masuala muhimu, kwa mfano, makubaliano ya usafirishaji nafaka.”

Kwenye mkutano katika kikao cha mashauriano, Putin anatarajiwa kutoa “taarifa muhimu” kwamba atazungumzia suala la chakula na mbolea, mshauri wa mambo ya nje wa Kremlin Yuti Ushakov alisema kama alivyokaririwa na mashirika ya habari ya Russia.

Rais Vladimir Putin
Rais Vladimir Putin

“Mtizamo mkuu utakaotupiwa jicho sana itakuwa ni matarajio kwa maendeleo zaidi ya uhusiano kati ya Afrika na Russia msisitizo ukiwa msaada wetu kwa maendeleo ya kitaifa ya waafrika, kuhakikisha fursa ya haki katika kupata chakula, mbolea, teknolojia ya kisasa na rasilimali za nishati,” Ushakov alisema.

Putin atafanya mikutano kadhaa na viongozi mbali mbali wa kiafrika, wakiwemo marais wa Cameroon, Senegal, Afrika Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa mujibu wa Ushakov.

“Jukumu la Afrika limeongezeka. Tumeona mawasiliano kadhaa yakiongezeka kwa kiwango cha juu na katika ngazi ya juu. Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov alifanya ziara kadhaa barani Afrika. Vladimir Putin alikutana na viongozi wa nchi za Afrika mara kwa mara. Kwahiyo, jukumu la Afrika linaongezeka. Mahitaji kwa msimamo wa kiafrika kuhusu hali ya sasa kwenye uwanja wa dunia nayo pia inakua,” anaendelea kusema Sviridov.

Mkutano huu ni wa pili wa aina yake baada ya ule wa kwanza ambao ulifanyika mwaka 2019 huko Sochi, kusini mwa Russia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG