Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:37

Ndege ya kivita ya Russia yairushia baruti droni ya Marekani Syria

Ndege ya kivita ya Russia ikiruka karibu ikihatarisha usalama wa ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani MQ-9 kabla ya kuirushia baruti droni ya Marekani ambayo ilikuwa na shughuli maalum huko Syria Julai 23, 2023.(Picha kwa hisani ya Jeshi la Anga la Marekani).

Ndege ya kivita ya Russia iliruka umbali wa mita chache kutoka katika ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kwenye anga ya Syria na kupiga baruti.

Ndege hiyo iliipiga ndege ya Marekani na kuiharibu, jeshi la Marekani lilisema Jumanne, ikiwa ni tukio la karibuni katika mtiririko wa uchokozi wa Russia katika kuingilia kati droni za Marekani zinazoruka katika eneo hilo.

Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Anga alisema hatua hiyo iliyotokea Jumapili ilikuwa ni jaribio la Russia kuiangusha droni ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper kutoka angani na imekuja wiki tu baada ya ndege ya kivita ya Russia kuruka karibu ikihatarisha usalama wa ndege ya uchunguzi ya Marekani inayosafirisha wafanyakazi katika eneo, ikihatarisha maisha ya Wamarekani wanne waliokuwa ndani yake.

“Moja ya fataki zilizopigwa na Russia ziliigusa droni ya Marekani MQ-9, na kuharibu panga boi lake,” Lt. Jenerali Alex Grynkewich, mkuu wa Majeshi ya Anga ya Marekani Kati, alisema katika taarifa iliyo elezea wito wa hivi karibuni.

Picha ya panga boi ya droni ya Marekani aina ya US MQ-9 iliyopigwa na fataki kutoka ndege ya kivita ya Russia ikiruka karibu na droni hiyo katika anga ya Syria Julai 23, 2023.
Picha ya panga boi ya droni ya Marekani aina ya US MQ-9 iliyopigwa na fataki kutoka ndege ya kivita ya Russia ikiruka karibu na droni hiyo katika anga ya Syria Julai 23, 2023.

“Tunatoa wito kwa majeshi ya Russia huko Syria kuacha mara moja uzembe huu, unaofanywa bila ya uchokozi na tabia isiyokuwa na weledi.

Grynkewich alisema mmoja wa wafanyakazi wanaoendesha droni hizo ardhini aliiweka hewani na kuirusha kurejea katika kituo chake.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG