Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:58

Ukraine yaomba ndege za kivita kwa Ufaransa


Waziri wa ulinzi wa Ukraine, Oleksii Reznikov, alitembelea Paris kwa mazungumzo na viongozi wa Ufaransa, Jumanne, ya kutoa msukumo wa kupata ndege za kivita kusaidia Kyiv kukabiliana na uvamizi wa Russia wa mwaka mzima.

Maafisa wa Ukraine wametoa mwito kwa washirika wake wa magharibi kupeleka ndege ili kupambana na mashambulizi ya Russia, lakini mpaka sasa mwito huo umekabiliwa na hali ya wasiwasi.

Alipoulizwa na wanahabari kama Ufaransa inafikiria kupeleka ndege za kivita Ukraine, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Jumatatu alisema kwamba hakuna kitu kilichoachwa, lakini akaelezea masharti kadhaa kabla ya jambo hilo kufanyika.

Yanajumulisha ndege kutogusa ardhi ya Russia, na kusababisha kuongeza mtafaruku na kwamba haita dhoofisha uwezo wa jeshi la Marekani. Rais wa Marekani, Jumatatu alisema Marekani haitapeleka ndege zake za F-16, Ukraine.

XS
SM
MD
LG