Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:45

Korea Kaskazini inamkaribisha Waziri wa ulinzi wa Russia na wengine kutoka China


Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Shoigu
Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Shoigu

Russia moja ya washirika wa kihistoria wa Pyongyang anaendelea kuwa moja ya mataifa machache yanayodumisha uhusiano wa kirafiki na Korea Kaskazini na kiongozi wake Kim Jong Un, ambaye hivi karibuni ameelezea uungaji mkono wake Moscow kuivamia Ukraine

Korea kaskazini wiki hii itamkaribisha waziri wa ulinzi wa Russia na ujumbe wa ngazi ya juu wa China mjini Pyongyang kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya vita vya Korea, vyombo vya habari vya serikali vimesema Jumanne ikionyesha ishara kwamba inaweza kufungua tena mipaka yake kwa wageni wa ngazi ya juu baada ya kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la virusi vya corona.

Ujumbe wa kijeshi wa Shirikisho la Russia ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, utafanya ziara ya pongezi kwa DPRK, Shirika la Habari la Korea lilisema siku moja baada ya kuthibitisha ujumbe wa China, pia utahudhuria hafla hiyo ya Alhamisi.

Russia moja ya washirika wa kihistoria wa Pyongyang anaendelea kuwa moja ya mataifa machache ambayo yanadumisha uhusiano wa kirafiki na Korea Kaskazini na kiongozi wake Kim Jong Un, ambaye hivi karibuni ameelezea uungaji mkono wake Moscow kuivamia Ukraine, ikiijumuisha Washington, anasema sambaza roketi na makombora.

China mshirika mkuu wa kibiashara wa Korea Kaskazini pia imethibitisha Jumanne kwamba itapeleka ujumbe unaoongozwa na mwanachama wa Politburo, Li Hongzhong.

Wageni hao wa nchi za nje wanatarajiwa kuhudhuria hafla mjini Pyongyang kuadhimisha miaka 70 tangu kutiwa saini kwa mkataba wa kusitisha mapigano unaojulikana kama Victory Day huko Kaskazini ambapo KCNA inasema itaadhimishwa kwa matukio mazuri ambayo yatawekwa katika historia.

Forum

XS
SM
MD
LG