Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:19

Serikali ya Marekani yaweka vikwazo kwa  maafisa watatu wa Mali

Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara akikagua gwaride la wanajeshi kabla ya mkutano na mwenzake wa Ufaransa Florence Parly, mjini Paris, Jumatano, Januari 27, 2021.(AP)
Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara akikagua gwaride la wanajeshi kabla ya mkutano na mwenzake wa Ufaransa Florence Parly, mjini Paris, Jumatano, Januari 27, 2021.(AP)

Serikali ya Marekani siku ya Jumatatu iliweka vikwazo kwa  maafisa watatu wa Mali akiwemo waziri wa ulinzi kwa tuhuma za kufanikisha kupelekwa  na kuongeza shughuli za Kundi la Wagner la Russia katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Wizara ya Fedha ya Marekani imesema imemuwekea vikwazo Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara, ambaye ilisema alifanya safari kadhaa nchini Russia mwaka 2021 ili kuimarisha makubaliano kati ya Kundi la Wagner na serikali ya mpito ya Mali ya kupeleka kikosi cha mamluki.

Vikwazo hivyo vya Jumatatu pia vinawalenga Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Mali Alou Boi Diarra na Naibu Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Mali Adama Bagayoko wizara hiyo ilisema.

Maafisa hawa wamewaweka watu wao katika hatari ya kuathiriwa na shughuli za Kundi la Wagner na ukiukaji wa haki za binadamu huku wakifungua njia ya unyonyaji wa rasilimali za nchi yao kwa manufaa ya shughuli za Kundi la Wagner nchini Ukraine naibu waziri wa Fedha anyeshughulkikia Ugaidi na Ujasusi wa Fedha Brian Nelson alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG