Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:16

Russia imepata mafanikio kiasi kaskazini mwa Ukraine; Inasema ripoti ya Uingereza


Mojawapo ya ndege za kivita za Russia
Mojawapo ya ndege za kivita za Russia

Vikosi vya Russia vinaweza kurudi kwenye Mto Oskil kuunda eneo la ulinzi kuzunguka Luhansk kwa sababu liko chini yake, wizara ya ulinzi ya uingereza ilisema, bila shaka ni moja ya malengo ya msingi ya vita vya Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Jumapili katika ripoti yake ya kila siku ya ujasusi kuhusu Ukraine kwamba Russia imepata mafanikio kiasi kaskazini mwa Ukraine huko Luhansk na Kharkiv, lakini hali hiyo imefichwa na habari za Russia.

Harakati hiyo, wizara ya Uingereza imesema, inaangazia umuhimu wa kaskazini kwa Russia, wakati Russia pia inakabiliwa na shinikizo kubwa katika eneo la kusini la Zaporizhzhia.

Vikosi vya Russia vinaweza kurudi kwenye Mto Oskil kuunda eneo la ulinzi kuzunguka Luhansk kwa sababu liko chini yake, wizara hiyo ilisema, bila shaka ni moja ya malengo ya msingi ya vita vya Russia.

Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alizungumza Jumamosi na mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg kuhusu njia za kurejesha usafiri salama wa meli zinazobeba nafaka za Ukraine kupitia Black Sea.

Forum

XS
SM
MD
LG