Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:42

Zelenskyy anasema daraja la Crimea ni lengo halali huku Ukraine ikikanusha shambulizi


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy

Akizungumza Ijumaa kwa njia ya video iliyounganishwa na Aspen Security Conference nchini Marekani, Zelenskyy alisema hii ni njia iliyotumiwa kuendesha vita kwa silaha na hii imekuwa ikifanywa kila siku

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy alisema Ijumaa kwamba daraja la Crimea ni lengo halali. Daraja ambalo linaunganisha Crimea kwenda Russia lilishambuliwa siku ya Jumatatu kwa milipuko ambayo iliuwa watu wawili. Kufuatia shambulizi hilo sehemu ya daraja lilikatika.

Akizungumza Ijumaa kwa njia ya video iliyounganishwa na Aspen Security Conference nchini Marekani, Zelenskyy alisema hii ni njia iliyotumiwa kuendesha vita kwa silaha na hii imekuwa ikifanywa kila siku. Inaifanya Peninsula ya Crimea kuwa ni eneo la kijeshi. Ukraine haijadai kuhusika kwa shambulizi kwenye daraja hilo. Moscow inaishutumu Ukraine.

Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya kila siku hapo Ijumaa, Russia iliwauwa watoto wawili zaidi hivi leo, msichana aliyezaliwa mwaka 2007 na mvulana aliyezaliwa 2013 walifariki. Alisema watoto hao waliuawa katika shambulizi moja kwenye kijiji cha Druzhba katika mkoa wa Donetsk.

Wanawake wawili pia waliuawa katika shambulizi hilo huku kituo kimoja cha kitamaduni, shule na majengo ya makaazi yaliharibiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG