Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:26

Russia inasema vikosi vyake vilishambulia kituo cha Dnipro nchini Ukraine


Jengo la makaazi lililoharibiwa na shambulizi la kijeshi la Russia huko Dnipro
Jengo la makaazi lililoharibiwa na shambulizi la kijeshi la Russia huko Dnipro

"Jioni ya Julai 28, vikosi vyenye silaha vya Russia vilishambulia kituo cha kamandi ya kikosi chenye silaha cha Ukraine katika mji wa Dnepropetrovsk kwa silaha za kiwango cha juu", wizara ya ulinzi ya Russia ilisema, ikiitaja Dnipro kwa jina lake la awali. Malengo yaliyotengwa yamefikiwa

Russia imesema Jumamosi kwamba vikosi vyake vilishambulia kituo cha kamandi huko Dnipro nchini Ukraine siku moja baada ya Kyiv kusema kombora lilipiga jengo moja la makaazi na kuwajeruhi watu tisa.

"Jioni ya Julai 28, vikosi vyenye silaha vya Russia vilishambulia kituo cha kamandi ya kikosi chenye silaha cha Ukraine katika mji wa Dnepropetrovsk kwa silaha za kiwango cha juu", wizara ya ulinzi ya Russia ilisema, ikiitaja Dnipro kwa jina lake la awali. Malengo yaliyotengwa yamefikiwa.

Maafisa wa Kyiv walisema Ijumaa kuwa kombora la Russia lilipiga jengo la makaazi huko Dnipro siku ya Ijumaa na kuwajeruhi watu tisa wakiwemo watoto wawili. Maafisa wanasema majengo mengine kadhaa yalishambuliwa ikiwemo jengo lisilokuwa na watu linalomilikiwa na idara ya usalama nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG