Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:25

Putin aahidi kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kisiasa na Afrika


Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na baadhi ya viongozi wa kiafrika waliohudhuria kikao
kwenye mji wa Saint Petersburg, Russia.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na baadhi ya viongozi wa kiafrika waliohudhuria kikao kwenye mji wa Saint Petersburg, Russia.

Akihutubia mkutano wa siku mbili wa kilele wa Russia na Afrika, Putin alisisitiza kuwa Moscow itatathmini kwa kina, pendekezo la amani kwa Ukraine, ambalo viongozi wa Afrika wamekuwa wakitoa.

Mkutano huo wa ulifunguliwa Alhamisi mjini St Petersburg, Russia ikiwa chini ya wiki mbili tangu taifa hilo lilipojiondoa kwenye mkataba wa nafaka wa Black Sea. Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema leo Ijumaa kwamba ni viongozi 17 pekee waliohudhuria mwaka huu ikilinganishwa na 47 waliohudhuria kikao kilichopita.

Kabla ya Russia kujiondoa kwenye mkataba huo, tani milioni 30 za nafaka kutoka Ukraine zilipelekwa barani Afrika, wizara hiyo imeongeza, wakati ikitoa ripoti ya kila siku kuhusiana na uvamizi wa Russia wa Ukraine. Imeongeza kusema kwamba kando na kusababisha kupanda kwa bei za vyakula, hatua hiyo ya Russia pia itasababisha ukosefu wa usalama wa chakula kote barani Afrika, kwa takriban miaka miwili ijayo.

Wakati huo huo shirika la habari la BBC limesema kwamba limetoa picha ya kiongozi wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin aliyeongoza jaribio la mapinduzi nchini Russia mwezi uliopita. Ripoti zimeongeza kwamba kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kutambua sura, wameweza kudhibitisha picha ya Prigozhin wakiwa na Freddy Mapuol ambaye ni afisa wa ngazi ya juu kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, anayehudhuria kongamano la Russia na mataifa ya kiafrika.

Forum

XS
SM
MD
LG