Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:40

Russia inahamu ya kuimarisha uhusiano na Afrika -Putin


Rais wa Russia Vladimir Putin akiongoza kifungua kinywa akiwa na wakuu wa mashirika ya kanda ya Afrika huko Saint Petersburg Julai 27, 2023. Picha na Valery SHARIFULIN / AFP.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiongoza kifungua kinywa akiwa na wakuu wa mashirika ya kanda ya Afrika huko Saint Petersburg Julai 27, 2023. Picha na Valery SHARIFULIN / AFP.

Rais wa Russia Vladimir Putin amewaambia viongozi wa Afrika siku ya Alhamis katika mkutano unaofanyika huko St. Petersburg kuwa Moscow iko tayari kufanya kazi na viongozi wa Afrika kwa maendeleo yao ya kifedha, na kutumia sarafu za nchi zao kwa malipo ya kibiashara.

Akihutubia mkutano huo wa Russia na Afrika Rais Putin alisema Russia ilikuwa na hamu kubwa ya kuimarisha uhusiano na bara la Afrika na ana imani huenda hilo litaongeza biashara.

Mkutano huo ambao unakuja baada ya Moscow kujiondoa katika makubaliano ambayo yalihusu bahari ya Black Sea itumike katika kusafirisha nafaka, ambazo ni muhimu kwa nchi za Afrika, hatua ambayo imeshutumiwa vikali kote duniani na kuleta tishio jipya kwa usalama wa chakula ulimwenguni.

Akizungumza katika mkutano huo, Azali Assouamani ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro alisema kwamba nchi za kiafrika zinawasihi wadau katika makubaliano ya nafaka kati ya Ukraine na Russia kutafuta njia muafaka ili kuruhusu nafaka hizo zitiririke na kufika barani Afrika.

Alisema “Makubaliano kuhusu usafirishaji wa nafaka lazima uwezekane ili kujaribu kuokoa maelfu ya watu ambao wanategemea nafaka hizi kutoka nje. Uchumi wa usalama wa chakula wa Afrika utakuwa katika hatari kubwa, hasa kwa vile bara hilo tayari limeathiriwa vibaya na bei kubwa za chakula ambazo zimesababishwa na kuvurugika kwa usambazji wa chakula.”

Na aliongeza kuwa “Kwahiyo, tunawasihi wadau kutafuta njia muafaka kuruhusu kuanza tena shughuli hiyo, kufikisha nafaka hizo za Ukraine na Russia katika bara letu.”

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa Saint Petersburg Julai 27, 2023.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa Saint Petersburg Julai 27, 2023.

Naye Rais Putin alisema upanuzi zaidi wa biashara na uhusiano wa kiuchumi na nchi za Afrika, ilikuwa muhimu kuingia katika mawasiliano ya kibiashara kuhusu sarafu za kitaifa, ikiwa ni pamoja sarafu ya ruble, katika malipo ya kifedha.

“Kupanua wigo zaidi wa kibiashara na uhusiano wa kiuchumi, ni muhimu kuwa na mawasiliano yenye nguvu ya kibiashara kwa kutumia sarafu za kitaifa za kila nchi, ikiwa ni pamoja na rubble, katika mawasiliano yoyote ya kibiashara. Kuhusiana na hili, tuko tayari kufanya kazi na nchi za kiafrika ilikuendelea miundo mbinu ya kifedha, kuwa na muingiliano na taasisi za kibenki kuhusu mfumo wa malipo ambao umetengenezwa na Russia, ambao utaruhusu malipo yatakayofanywa bila ya kujali ni sarafu gani iliyopo inayotumika na kuweka kiwango kwa mifumo ya Magharibi. Hii itaimarusha uthabiti na usalama wa mahusiano sawa ya kibiashara.” Alisema Putin.

Wakati huo huo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Azali Asouamani alisema umoja huo umelaani mapinduzi ya Niger baada ya wanajeshi waasi kudai kumuondoa madarakani Rais Mohammed Bazoum.

Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na Rais wa Comoro Azali Assoumani huko Saint Petersburg Julai 27, 2023.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na Rais wa Comoro Azali Assoumani huko Saint Petersburg Julai 27, 2023.

Alisema ameungana na Umoja wa Afrika, “katika kulaani kilichotokea Niger na kupendekeza kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba na kuachiliwa kwa Rais Bazoum na familia yake.”

“Najiunga na Umoja wa Afrika, taarifa iliyotolewa na jumuiya, inalaani kilichotokea nchini Niger na kupendekeza kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba na kuachiliwa kwa Rais Bazoum na familia.” Alisema Assoumani.

Jumatano asubuhi, wanachama wa kikosi cha ulinzi wa rais kiliizingira nyumba ya Bazoum na mke wake akiwa ndani wakiwazuia humo.

Wanajeshi waasi, ambao wanajiita wenyewe kuwa Baraza la Kitaifa katika Kuilinda Nchi, walikwenda kwenye kituo cha taifa cha televisheni na kutangaza kuwa wamekamata udhibiti kwasababu ya kushuka kwa usalama na uchumi mbaya na utawala wa kijamii katika taifa hilo lenye takriban watu milioni 25.

Lakini serikali ya Niger ilisema kamwe haitakubali utawala wao na kuwataka wananchi kulikataa hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG