Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:32

Kiongozi wa Korea Kaskazini apokea ujumbe wa Russia na China katika kilele cha sherehe za miaka 70

Picha imetolewa na serikali ya Korea Kaskazini, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, kulia, akiwa na ujumbe wa Russia ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu wakitembelea maonyesho ya silaha huko Pyongyang, Korea Kaskazini, Julai 26, 2023.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amepokea ujumbe wa kijeshi wa Russia na ujumbe wa kisiasa wa China katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya ushindi uliotangazwa na taifa hilo maarufu kama “Victory Day.”

Kim ametumia sherehe hizo kwa ajili ya kujenga diplomasia baada ya miaka kadhaa ya kujitenga kwasababu ya masharti makali ya kudhibiti COVID-19.

Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu na mjumbe wa Politiburo ya China Li Hongzhong waliwasilisha barua kwa Kim kutoka kwa viongozi wao, Vladimir Putin na Xi Jinping, chombo cha habari cha serikali KCNA kilisema Alhamisi.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (kati), Mjumbe wa Politiburo ya Chama cha Kikomunisti cha China Li Hongzhong (wanne kulia) na Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu (kushoto) wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya vita huko Pyongyang, Julai 27, 2023. (Korean Central News Agency)

Kilisema kuwa Kim alipokea barua kwa shukrani kubwa, akielezea urafiki wa miongo mingi kati ya nchi zao.

Wajumbe hao walikaribishwa na Kim katika maonyesho ya muziki baada ya saa sita usiku, ambapo yaliadhimisha ushindi unaodaiwa kwa muda mrefu na taifa hilo dhidi ya “uvamizi wa kijeshi uliofanywa na ubeberu wa Kimarekani.

Vita vya Korea vya 1950-53 vinaelezewa kuwa ni vita vya ukombozi wa ardhi baba huko Korea Kaskazini, mapigano ya umwagaji damu ambayo kimakosa yalichochewa na Marekani na washirika wake.

Maadhimisho hayo ya miaka 70 ni ambayo Pyongyang wanahitaji kujipamba na hatua muhimu ya mafanikio.

Forum

XS
SM
MD
LG