Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:00

Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo wahusika wakuu katika vita vya Sudan


Moshi ukifuka kusini mwa jiji la Khartoum, Juni 12, 2023. Picha na AFP.
Moshi ukifuka kusini mwa jiji la Khartoum, Juni 12, 2023. Picha na AFP.

Umoja wa Ulaya hatimaye umeanzisha mfumo maalum wa vikwazo vinavyowalenga wahusika wakuu katika vita vya Sudan vinavyoendelea, kwa kuwawekea vizuizi vya kusafiri na mali zao ikiwemo kuwafungia akaunti za benki, vyanzo vya kidiplomasia vinavyofahamu suala hilo vimesema.

Hati ya pendekezo iliyotumwa kwa nchi wanachama mwishoni mwa wiki iliyopita, na maelezo zaidi kuhusu suala hilo yatajadiliwa wiki zijazo, vyanzo vya kidiplomasia vilisema. Lengo ni kumaliza muundo wa kazi ifikapo Septemba, baada ya hapo unaweza kutumika kutengeneza orodha ya watu binafsi na makampuni yaliyopigwa marufuku, vyanzo vilisema.

Mapema mwezi Mei, rais wa Marekani Joe Biden alitia saini amri ya kiutendaji ili kuweka msingi kwa uwezekano wa vikwazo vya Marekani.

EU tayari imeyawekea vikwazo mashirika na watu binafsi wanaohusishwa na kundi la mamluki la Wagner la Russia, linaloongozwa na Yevgeny Prigozhin, zikiwemo shughuli zake nchini Sudan pamoja na makampuni mawili ya dhahabu.

Vita vilizuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu kati ya jeshi, likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye alimuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir mnamo 2019, na kikosi cha wanamgambo kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti.

Hemedti alipata utajiri wake kutoka kwenye migodi ya dhahabu huko Darfur na vikosi vya msaada wa dharura (RSF) vina uhusiano wa karibu na Saudi Arabia yenye nguvu katika Ghuba na Umoja wa Falme za Kiarabu. Wakati jeshi la Burhan linaungwa mkono na wafuasi wa Kiislamu wa Bashir.

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, alionya mwezi Julai kuwa mzozo hauonyeshi dalili za haraka za kuleta suluhisho na "kuhatarisha kubadilika kwa vita hivyo na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe” na masitisho ya mapigano yamekuwa yakitumiwa na pande zote mbili kujipanga upya.

Mapema mwezi huu, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji linakadiria kuwa watu milioni tatu wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano, na zaidi ya watu 700,000 wamekimbilia nchi jirani kama vile Misri na Chad. Wakati huo huo mgogoro wa kibinadamu umekuwa ukiongezeka kutokana na misaada kushindwa kufiia katika maeneo yaliyokusudiwa.

Chanzo cha habari hii nia shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG