Karim Khan ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mahakama ya ICC ina mamlaka ya kuchunguza uhalifu uliofanywa Darfur na kwamba inachunguza vurugu zilizotokea huko tangu mapigano yalipoanza April 15 kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha jeshi la dharura RSF.
Kumekuwepo na ripoti kadhaa za vurugu dhidi ya raia hasa katika mji wa El Geneina, huko Darfur Magharibi.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba kikosi cha jeshi la dharura RSF na makundi ya wanamgambo, wanahusika na kaburi la pamoja ambalo limegunduliwa huko.
Karim Khan amesema kwamba hatua zinastahili kuchukuliwa dhidi ya wahusika na wala kuongea tu, wala kutoa kibali cha wahusika kukamatwa, lakini kuhakikisha kwamba haki inapatikana na kujenga Imani kwa watu wa Dafur kwamba Maisha yao ni muhimu.
Forum