Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:56

Misaada ya kibinadamu Sudan huwenda ikasitishwa kutokana na mashambulizi;MSF


Nembo ya shirika la madaktari wasio na mipaka (MSF)
Nembo ya shirika la madaktari wasio na mipaka (MSF)

Shirika la madaktari wasio na mipaka (MSF) lilisema wafanyakazi wake wanne, madereva wake wane na wafanyakazi kumi wa kila siku waliokuwa wakipeleka vifaa vya dawa kwenye hospitali ya Turkish mjini Khartoum siku ya Alhamis walisimamishwa na kushambuliwa vibaya

Shirika la madaktari wasio na mipaka linasema halitaweza kuendelea na kazi yake katika moja ya hospitali mbili pekee ambazo bado ziko wazi katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kama uhakikisho wa usalama wa kiwango cha kawaida hautatekelezwa.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, shirika hilo linalojulikana kwa kifupi MSF ilisema kwamba wafanyakazi wake wanne, madereva wake wane na wafanyakazi kumi wa kila siku ambao walikuwa wakipeleka vifaa vya dawa kwenye hospitali ya Turkish mjini Khartoum siku ya Alhamis walisimamishwa na kushambuliwa vibaya na wanaume wenye silaha ambao waliiba gari la wafanyakazi hao.

Iwapo tukio kama hili linatokea kwa mara nyingine, na kama uwezo wetu wa kupeleka vifaa unaendelea kuzuiliwa, kwa masikitiko, uwepo wetu katika hospitali ya Turkish hautakuwepo hivi karibuni, Christophe Garnier meneja wa kitengo cha dharura katika MSF kwa Sudan alisema katika taarifa.

Mamilioni ya watu wamekimbia nyumba zao tangu mapigano yalipozuka nchini Sudan, katikati ya April kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces mjini Khartoum na kwingineko huko Sudan.

Forum

XS
SM
MD
LG