Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:54

Shambulizi la roketi limeua raia 16 katika mkoa wa Darfur nchini Sudan


Mfano wa maeneo yaliyoharibiwa kwa vita huko El Geneina mji mkuu wa West Darfur. April 29, 2023
Mfano wa maeneo yaliyoharibiwa kwa vita huko El Geneina mji mkuu wa West Darfur. April 29, 2023

Eneo hilo kubwa ambalo tayari limeharibiwa na vita vya kikatili mwanzoni mwa miaka ya 2,000 limeshuhudia baadhi ya ghasia mbaya sana tangu mapigano yalipozuka katikati ya mwezi Aprili kati ya majenerali wanaohasimiana wa Sudan wanaowania madaraka

Raia wasiopungua 16 wameuawa kwa shambulizi la roketi ambalo limepiga nyumba zao katika mkoa wa Darfur, magharibi mwa Sudan chama cha wanasheria katika eneo kilisema Jumamosi.

Eneo hilo kubwa ambalo tayari limeharibiwa na vita vya kikatili mwanzoni mwa miaka ya 2,000 limeshuhudia baadhi ya ghasia mbaya sana tangu mapigano yalipozuka katikati ya mwezi Aprili kati ya majenerali wanaohasimiana wa Sudan wanaowania madaraka.

Wakati wa majibizano ya roketi kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) raia 16 waliuawa siku ya Ijumaa kulingana na idadi ya awali, huko Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini chama cha wanasheria kilisema.

Angalau mtu mmoja aliuawa na mlenga shabaha iliongeza taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG