Anahojiwa kutokana na matamshi yake yanayoelezwa kuwa yanaweza kueneza chuki dhidi ya raia wa kigeni wanaofanya shughuli za biashara nchini humo.
Jaguar, anadaiwa kusema kwamba Wakenya wanastahili kutumia nguvu kuwafurusha raia wa kigeni, matamshi ambayo serikali ya Kenya imejitenga nayo, na kuzuwa mjadala mkubwa katika nchi za Afrika Mashariki.