Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:26

Pande hasimu Sudan zapambana Khartoum baada mazungumzo kuvunjika, hali iliyochochea Marekani kuweka vikwazo


Mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada ya kibinadamu la Premiere Urgence akiwasaidia wakimbizi wa Sudan kuvuka mpaka kwenda Chad. Tarehe 1, Mei 2023. Picha na Gueipeur Denis SASSOU / AFP.
Mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada ya kibinadamu la Premiere Urgence akiwasaidia wakimbizi wa Sudan kuvuka mpaka kwenda Chad. Tarehe 1, Mei 2023. Picha na Gueipeur Denis SASSOU / AFP.

Pande zinazopigana nchini Sudan zimepambana katika mji mkuu kwa usiku mzima mpaka leo asubuhi baada ya mazungozmo yanayolenga kuendeleza sitisho la mapigano na kupunguza mzozo wa kibinadamu kuvunjika, na kuichochea Marekani kuweka vikwazo.

Wakazi wa Khartoum na mji jirani wa Omdurman wamesema jeshi limeanza mashambulizi ya anga na wanatumia mizinga zaidi wakati mapambano yakiendelea, bila ya dalili kwamba kikosi cha RSF kitaondoka katika mitaa na nyumba mjini humo.

Wiki saba za mapigano kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces zimeharibu sehemu na katikati mwa Khartoum, kutishia utulivu katika eneo kubwa, watu milioni 12 kuksoeshwa makazi ndani ya Sudan na kupelekea watu wengine laki nne kukimbilia katika mataifa jirani.

Marekani na Saudi Arabia jana Alhamisi zilisitisha mazungumzo ya amani baada ya sitisho la mapigano ambalo walisimamia lilivunjika, na kuzishutumu pande zote mbili kuvamia nyumba, biashara na mahospitali, na kufanya mashambulizi ya anga na kuweka za harakati za kijeshi.

Washington iliweka vikwazo kwa biashara ambazo zinahusishwa na jeshi na RSF na kutishia kuchukua hatua zaidi, “kama pande hizo zitaendelea kuiharibu nchi yao,” kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Marekani.

Jenerali Abdel-Fattah Burhan
Jenerali Abdel-Fattah Burhan

Balozi wa Sudan kwa Washington, Mohammed Abdallah Idris, alisema serikali yake na jeshi bado wana nia ya dhati kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na adhabu zozote ni vyema “ziwekwe kwa pande ambazo hazikuhesimu kile ambacho walitia saini,” – akikizungumzia kikosi cha RSF.

Pande hizo mbili zimelaumiana kila mmoja kwa kukiuka sitisho la mapigano.

Hali ya kibinadamu nchini Sudan ni janga kubwa, afisa wa shirika la mpango wa chakula duniani – WFP alisema Alhamisi, akielezea kuwa watu zaidi ya milioni 10 katika nchi hiyo wanakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa chakula.

“Hali ya kibinadamu ni janga nchini Sudan, hasa katika maeneo kama vile Khartoum na majimbo ya magharibi. Tunafahamu kwamba kabla ya vita, kulikuwa na watu milioni 15 ambao walikuwa wanakabiliwa na ukosefu wa chakula. Pia tunafahamu kwamba idadi hii imeongezeka kwa mamilioni baada ya kuanza. Watu wana shida ya msaada wa chakula pamoja nahuduma za afya. Tunafahamu kwamba zaidi ya watu milioni moja wamekimbia kutoka maeneo yenye mizozo, ama kwa kuvuka mipaka au kuhamia majimbo mengine ambayo ni salama kwao,” amesema Mohamed Gamal, Afisa Mawasiliano, wa WFP.

Watu wakinunua vyakula sokoni huko kusini mwa jiji la Khartoum, wakati mapigano yalipositishwa, tarehe 31 Mei. Picha na AFP.
Watu wakinunua vyakula sokoni huko kusini mwa jiji la Khartoum, wakati mapigano yalipositishwa, tarehe 31 Mei. Picha na AFP.

Kote nchini Sudan, shirika hilo limewafikia zaidi ya watu laki saba na elfu 82 kwa kuwapatia chakula na lishe katika muda wa wiki nne zilizopita.

Huduma za dharura za mawasiliano za WFP kwa mashirika yote ya Umoja wa Mataifa na jamii pana ya kibinadamu bado ni changamoto kubwa nchini Sudan.

“Huku mzozo ukiendelea na sitisho la mapigano likiwa halijaa vyema, inafanya iwe vigumu sana kwetu sisi, na wahusika wa misaada wa kibinadamu, kusambaza misaada na misaada mingine ya kuokoa maisha kwa wale ambao wana shida tungependa kuona sitisho hili la mapigano linatekelezwa vyema na haraka vita visimame, ili tuweze kuokoa hali ya kibinadamu inayozidi kudorora kwasababu ya vita, siyo tu Khartoum lakini katika maeneo mengine pia, hasa huko Darfu Magharibi ambako bado ni vigumu sana kufika kwasababu ya hali ya huko.”

Nje ya Khartoum, mapigano mabaya zaidi yanaendelea katika mkoa wa Darfur, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vikiendelea tangu mwaka 2003, na kusababisha vya takriban watu laki tatu.

Zaidi ya watu laki moja wamekimbia mashambulizi ya wanamgmabo huko Darfur Maghribi ambako ni jirani na Chad tangu mapigano ya karibuni yalipoanza, na idadi huenda ikaongezeka mara mbili zaidi katika miezi mitatu ijayo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limesema Alhamisi.

Forum

XS
SM
MD
LG