Hii ni baada ya wapatanishi wawili wakuu wa kimataifa kutoa ishara ya kutokuwepo na uvumilivu wa ukiukwaji wa mapatano ya amani.
Kuongezwa huko kwa siku tano za kusitisha mapigano baina ya jeshi la Sudan na wapinzani wake jeshi la akiba la RSF, kulitangazwa katika taarifa ya pamoja Jumatatu jioni ya Saudi Arabia na Marekani.
“Kuongezwa huko muda kutatoa wasaa wa misaada zaidi ya kibinadamu, kurejeshwa kwa huduma muhimu, na mjadala wa uwezekano wa kuongezwa kwa muda mrefu zaidi,” taarifa imeeleza.
Maendeleo yamefanyika baada ya zote Riyadh na Washington kuzitaja pande zote zinazo hasimiana Jumapili kwa ukiukwaji wa kusimamisha mapigano kwa wiki nzima ambalo kuliisha muda wake Jumatatu jioni.
Forum