Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:15

Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa pande zinazopigana Sudan


Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani, Jake Sullivan
Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani, Jake Sullivan

Marekani Alhamisi imetangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa Sudan inaowalaumu kwa kukwamisha makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyopatikana chini ya juhudi za Marekani na Saudi Arabia.

Marekani imetangaza vikwazo hivyo baada ya mashambulizi ya makombora na ya anga kuua raia 18 katika soko moja mjini Khartoum ambako mapigano yaliendelea leo Alhamisi baada ya jeshi kujiondoa kwenye mazungumzo ya amani.

Kwa zaidi ya wiki sita, Khartoum na maeneo mengine ya nchi yamekumbwa na vita vya umwagaji damu kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), Washington ikisema pande hizo mbili zimehusika kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano na kuchochea umwagaji damu wa kutisha.

“Tunafuatilia hali hiyo kwa kuweka vikwazo na vizuizi vya visa dhidi ya wahusika ambao wanaendeleza ghasia,” mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Jake Sullivan amesema katika taarifa.

“Raia 18 waliuawa na 106 kujeruhiwa” kwa shambulio la makombora na mashambulizi ya mabomu na ya anga Jumatano katika soko kusini mwa Khartoum, kamati ya wanasheria wa haki za binadamu imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG