Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:38

Watu 18 wauawa katika mashambulizi kwenye soko moja mjini Khartoum


Watu wakipita karibu na jengo la kituo cha matibabu kilichojaa matundu ya risasi kwenye soko liitwalo Souk Sitta, kusini mwa Khartoum, Juni 1, 2023
Watu wakipita karibu na jengo la kituo cha matibabu kilichojaa matundu ya risasi kwenye soko liitwalo Souk Sitta, kusini mwa Khartoum, Juni 1, 2023

Mashambulizi ya makombora na ya anga yaliua raia 18 katika soko moja mjini Khartoum nchini Sudan ambako mapigano yaliendelea leo Alhamisi baada ya jeshi kujiondoa kwenye mazungumzo ya amani.

Kwa zaidi ya wiki sita, Khartoum na maeneo mengine ya nchi yamekumbwa na vita vibaya kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).

Jumatano, jeshi lilishambulia kwa mabomu ngome za RSF mjini Khartoum baada ya kujiondoa kwenye mazungumzo ya huko Jeddan nchini Saudi Arabia, likimshutumu hasimu wake kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokusudia kuruhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

“Raia 18 waliuawa na 106 kujeruhiwa” kwa shambulio la makombora na mashambulizi ya mabomu kwa kutumia ndege Jumatano katika soko kusini mwa Khartoum, kamati ya wanasheria wa haki za binadamu imesema.

Idadi hiyo ya vifo imethibitishwa na kundi moja katika kitongoji cha Khartoum ambalo linagawa misaada ambalo limesema hali ilikuwa mbaya zaidi na kuomba msaada wa madkatari na damu.

Forum

XS
SM
MD
LG