Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:54

Sudan: Wapatanishi wanataka muda wa kusitisha vita kuongezwa


Wanajeshi wa Sudan wakipumzika kufuatia hatua ya kusitisha mapigano. Khartoum, May 25, 2023.
Wanajeshi wa Sudan wakipumzika kufuatia hatua ya kusitisha mapigano. Khartoum, May 25, 2023.

Marekani na Saudi Arabia zimetoa wito kwa pande zinazopigana nchini Sudan kuongeza muda wa kusitisha mapigano unaotarajiwa kumalizika kesho Jumatatu.

Wito huo umetolewa huku mapigano yakiwa yanaendelea kwa wiki kadhaa katika mji mkuu wa Khartoum na sehemu nyingine za nchi hiyo ya Afrika.

Jeshi la Sudan linapigana na kikosi cha jeshi la dharura RSF, kuwania uongozi wa Sudan.

Wamekuwa wakipigana tangu katikati mwa mwezi April.

Pande zote zilikuwa zimekubaliana wiki iliyopita, kusitisha mapigano kwa muda wa wiki moja, katika mazungumzo yaliyosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa makubaliano yaliyotangulia ya kusitisha vita, mapigano ya hapa na pale yamekuwa yakitokea Khartoum na sehemu nyingine za nchi.

Taarifa ya wapatanishi inataka vita kusitishwa ili wathirika kupata misaada ya kibinadamu, huku pande zinazopigana zikitakiwa kuendelea na mazungumzo.

Forum

XS
SM
MD
LG