Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:24

Jeshi la Sudan limewaita wanajeshi wa akiba na wastaafu, linataka mjumbe wa UN aondoke Sudan


Kamanda wa jeshi la Sudan Gen. Abdel Fattah al-Burhan
Kamanda wa jeshi la Sudan Gen. Abdel Fattah al-Burhan

Jeshi la Sudan limewataka wanajeshi wake wa akiba na waliostaafu kurudi kazini, huku mapigano makali yakiendelea dhidi ya kikosi cha jeshi la dharura RSF, na kuitaka Marekani kumbadilisha balozi wake nchini humo.

Wito wa kutaka wanajeshi wa zamani kufika katika kambi yoyote ya jeshi iliyo karibu nao, inalenga kuimarisha nguvu ya jeshi la Sudan, katika mapigano dhidi ya RSF, lakini hatua hiyo inaweza kuongeza mapigano zaidi licha ya kutangaza kusitisha mapigano hayo.

Mapigano ya hapa na pale yamekuwa yakitokea wiki hii, japo waangalizi wa makubaliano ya kusitisha vita Saudi Arabia na Maarekani wamesema kwamba hali ilikuwa inaendelea kuwa nzuri japo hatua ya jeshi inaweza kuvuruga hali hiyo.

Msemaji wa jeshi la Sudan amesema kwamba wanajeshi wa akiba wametakiwa kujitolea na wala hawalazimishwi.

Kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fatteh al-Burhan, amemuandikia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akitaka kumbadilishwa kwa mjumbe wake, Volker Perthes.

Maelezo zaidi kuhusu yaliyomo kwenye barua hiyo hayajatolewa lakini Perthes, ambaye aliteuliwa mnamo mwaka 2021, alishinikiza kuundwa kwa serikali ya mpito inayoongozwa na raia, hatua ambayo baadhi ya viongozi wa kijeshi walipinga.

Forum

XS
SM
MD
LG