Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:48

Ndege ya kwanza yenye misaada yawasili Goma, DRC


Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini DRC Jean-Marc Chataigner na balozi wa Ufaransa nchini DRC Bruno Aubert wakiwa pamoja na gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Luteni Jenerali Constant Ndima Kongba, Machi 10, 2023. Picha na shirika la habari la REUTERS/Arlette Bashizi.
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini DRC Jean-Marc Chataigner na balozi wa Ufaransa nchini DRC Bruno Aubert wakiwa pamoja na gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Luteni Jenerali Constant Ndima Kongba, Machi 10, 2023. Picha na shirika la habari la REUTERS/Arlette Bashizi.

Ndege ya mizigo iliyobeba mahema, vifaa vya afya, na misaada mingine ya kibinadamu ilitua siku ya Ijumaa katika mji wa mashariki wa Goma huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Huu ni msaada wa kwanza kupelekwa huko chini ya mpango wa Umoja wa Ulaya (EU) ili kuwasaidia mamilioni ya watu waliokoseshwa makazi katika eneo hilo.

Mapigano kati ya jeshi la Kongo na M23, kundi la waasi ambalo linadai kuwakilisha maslahi ya watu wa kabila la Watutsi walioko mashariki mwa Congo. Mapigano hayo yamesababisha ongezeko la mzozo wa kibinadamu huku zaidi ya watu milioni 5.5 wakikoseshwa makazi katika majimbo kadhaa.

"Leo, watu hawa wanachokitaka ni amani ya kudumu ili waweze kurejea katika mazingira ya nyumbani kwao,” gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Constant Ndima Kongba, aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege.

Wiki iliyopita Umoja wa Ulaya uliahidi kupeleka misaada yenye thamani ya zaidi ya Euro milioni 47 ambazo ni sawa na dola milioni 50, huko Kivu Kaskazini kusaidia katika mahitaji ya haraka kama vile lishe, huduma za afya, maji na usafi wa mazingira, makazi na ulinzi.

Ndege ya pili iliyobeba vifaa vilivyotoka EU ilitarajiwa kuwasili wiki ijayo, amesema balozi wa EU kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean-Marc Chataigner, alipokuwa uwanja wa ndege wa Goma.

"Ni fursa nzuri kwetu kuonyesha mshikamano wa hali ya juu raia wa Kongo," alisema balozi huyo.

Ukosefu wa usalama katika eneo la mashariki mwa Congo umesambaa katika eneo hilo tete kwa zaidi ya mwaka mmoja, hali ambayo imesababisha na kuibuka tena kwa kundi la M23.

Eneo la mashariki mwa Congo limekuwa likipambana na ukosefu wa utulivu na migogoro tangu miaka ya 1990 ambapo mamilioni ya watu waliuwawa na kuibuka kwa makundi ya kadhaa ya wanamgambo, ambayo baadhi yao yanafanya harakati zao hadi hivi leo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG