Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:39

Waasi wa M23 wameshambulia wanajeshi wa Burundi, kambi ya wakimbizi, raia 2 wameuawa


Waasi wa M23 wakati walikuwa wanaondoka Kibumba, karibu na Goma, Kivu kaskazini, DRC, Dec. 23, 2022.
Waasi wa M23 wakati walikuwa wanaondoka Kibumba, karibu na Goma, Kivu kaskazini, DRC, Dec. 23, 2022.

Waasi wa M23 wameripotiwa kushambulia kambi ya wanajeshi wa Burundi waliowasili mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo siku chache zilizopita kwa ajili ya kulinda amani.

Ripoti zinasema kwamba mabomu 9 yamefyatuliwa na kundi hilo katika mji wa Sake, kilomita 15 kutoka mji wa Goma.

Shambulizi moja limepiga kambi ya wanajeshi wa Burundi na inahofiwa kwamba kuna wanajeshi wa wamefariki au kujeruhiwa japo mamlaka hawajatoa ripoti kamili.

Walioshuhudia wameambia idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kwamba raia wawili wameuawa.

Gavana wa Kivu kaskazini Kanali Kaiko Ndjike, ameambia gazeti la The east African kwamba waasi wa M23 wamekiuka mkataba wa kusitisha vita na kushambulia wanajeshi wa kulinda amani kutoka jumuiya ya Afrika mashariki, wa Burundi.

Shambulizi jingine limepiga kambi ya wakimbizi wa ndani.

Burundi: majibu yatakuwa mabaya na hatari kwa waasi wa M23

Katika taarifa, serikali ya Burundi imesema kwamba wanajeshi wake “wapo tayari kujibu shambulizi hilo na jibu lao linaweza kuwa baya zaidi na hatari kwa waasi hao.”

Waasi wa M23 walijaribu kudhibithi mji wa Sake kutoka kwa wanajeshi wa DRC bila mafanikio.

Hii ndio mara ya kwanza waasi wa M23 wameshambulia wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki walio DRC kwa ajili ya amani.

Wanajeshi wa Burundi wamepangiwa kushika doria katika miji ya Sake, Kirolirwe na Kitchanga, Kivu kaskazini, kulingana na makubaliano ya Addis Ababa, Februari 17, 2023.

Kenya ilikuwa nchi ya kwnza kutuma wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kulinda amani, kulingana na makubaliano ya viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Rais wa Rwanda Paul Kagame nayetuhumiwa kuunga mkono wasi wa M23
Rais wa Rwanda Paul Kagame nayetuhumiwa kuunga mkono wasi wa M23

Uganda na Sudan kusini kutuma wanajeshi

Uganda na Sudan kusini zinatarajiwa kutuma wanajeshi wake mashariki mwa DRC.

Wanajeshi wa Uganda watashika doria katika miji ya Bunagana, Kiwanja, Rutshuru na Mabenga, sehemu ambazo kwa sasa zinadhibitiwa na waasi wa M23.

Mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni, Generali Muhoozi Kainerugaba, amekuwa akiandika ujumbe wa twiter kila mara akisema kwamba wanajeshi wa Uganda hawatapigana na waasi wa M23 na kwamba waasi hao “ni ndugu wetu”.

Shambulizi dhidi ya wanajeshi wa Burundi linajiri saa chache kabla ya Angola, ambayo inatekeleza jukumu la upatanishi kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23, kusema kwamba waasi hao walikuwa wameahidi kusitisha mapigano kuanzia leo Jumanne March 7, 2023.

Shambulizi hilo pia limetokea muda mfupi baada ya serikali ya DRC kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na serikali ya Burundi.

Rwanda na DRC zinashutumiwa kuunga mkono makundi ya waasi

Waasi wa M23 wanadaiwa kupokea msaada wa serikali ya Rwanda, ambayo serikali ya DRC imekataa wanajeshi wake kuingia DRC.

Rwanda imekanusha kila mara kuwaunga mkono waasi wa M23 lakini inadai kwamba serikali ya DRC inaunga mkono waasi wa FDLR wanaotaka kupindua utawala wa rais Paul Kagame.

Ripoti ya wataalam wa umoja wa mataifa inasema kwamba Rwanda inatoa msaada wa kijeshi kwa waasi wa M23, na DRC inatoa msaada wa kijeshi kwa waasi wa FDLR.

Waasi wa M23 wameamurishwa na makamanda wa jeshi wa Afrika mashariki kuacha vita ifikapo March 30 na kuondoka Bunagana, Kiwanja na Rutshuru.

XS
SM
MD
LG