Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:36

M23 yatakiwa kuheshimu mkataba kusitisha mapigano


Waasi wa kundi la M23, tarehe 23, Desemba 2022. Picha na shirika la habari la AP /Moses Sawasawa.
Waasi wa kundi la M23, tarehe 23, Desemba 2022. Picha na shirika la habari la AP /Moses Sawasawa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito kwa waasi wa M23 nchini Jamhuri Kidemkorasi ya Congo (DRC) kuheshimu mkataba wa sitisho la mapigano unaotarajiwa kuanza kazi leo.

Antonio Guterres amekaribisha juhudi za kieneo na za kimataifa zinazongozwa na rais wa Angola na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kujaribu kuzuia mzozo ambao umewakosesha makazi maelfu ya watu hadi sasa.

Saa chache kabla ya sitisho la mapigano lililosimamiwa na Angola kuanza kufanya kazi, mapigano makali baina ya jeshi la Angola na kundi la M23 yameendelea kwenye jimbo la Kivu Kaskazini.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani ghasia zote dhidi ya raia na kuyasihi makundi yote yenye silaha kuweka silaha zao chini bila ya masharti.

Guterres amelitaka kundi la M23 kuheshimu ahadi ya kusitisha mapigano ili kufanikisha kikamilifu na kwa ufanisi kuondoka katika maeneo yote ambayo inayakalia kimabavu, baadhi yao karibu na Goma, mji mkubwa kabisa upande wa mashariki mwa nchi.

Ghasia zinazoendelea zimekosesha makazi maelfu ya watu katika mwaka uliopita na kupelekea shutuma kwamba Rwanda inawafadhili waasi, ambapo Kigali imekanusha shutuma hizo.

XS
SM
MD
LG