Kwa mujibu wa Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric Mkuu wa ujumbe wa kulinda amani huko DRC (MONUSCO), Bintou Keita kwa sasa yuko mashariki mwa nchi hiyo.
Alikutana na Gavana wa kijeshi wa jimbo la Ituri Jumatano ambaye ameomba msaada wa tume ya kulinda amani kuendelea kujenga uwezo wa vikosi vya usalama vya Congo.
Mapema wiki hii, alikutana na Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa ili kuimarisha ushirikiano na kutatua changamoto za usalama.
Bi Keita pia alishirikiana na wawakilishi wa mashirika ya kiraia na viongozi wanawake wanaokabiliwa na changamoto katika jamii zao.